06/01/2024
WAGENI WANAOKUJA MALINDI:
1) Ukitoka Mombasa kuja Malindi lazima upite daraja nne - Nyali, Shimo/Mtwapa, Mbogolo na Kilifi bridge.
2) Malindi kuingia ni harusi (rahisi), bali kutoka ni matanga (ngumu).
3) Mwanaharusi ni jina, sio mtoto aliyeolewa na harusi.
4) Beach si Bunthwani pekee, kuna Silversands, Dorado beach, Casino beach na Marine Park.
5) Kuna tofauti ya N**i, Dafu, Koroma na Mbata, chunga usitapeliwe.
6) Ukitaka kuuliza swali, salimia mtu kwanza, bila hivyo hujibiwi.
7) Misemo utakayoona kwenye LESO haikuhusu wewe.
8). Mwembe Tayari (KD) hakuna mwembe wowote.
9). Mwisho wa Malindi ni hapo Blue Marine. Barclays na 7to7 ziko Magarini.
10). Mugoka ni 50 bob
11). Malindi Mchana ni ndogo, lakini usiku kubwa.
12. Usidharau N**i, Maembe ni ya Msimu.
13. Na mtakapo rudi bara, DERA halivaliwi na sweta, mnaharibu mavazi.
KARIBUNI MALINDI๐