21/07/2026
`π UFUNUO SURA YA 7`
*Muhuri Atiao Mungu Katika Vipaji vya Nyuso za Watu Wake*
π Ufunuo 7:1-3:
> βBaada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote. Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari, akisema, Msiidhuru nchi wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyusi zao"
*_π Tulijifunza juu ya muhuri wa sita katika sura iliyopita. Muhuri wa saba haufunguliwi mpaka tunapofika sura ya nane. Kwa hiyo yanayotukia katika sura hii yanatokea kati ya kufunguliwa muhuri wa sita, na ule wa saba. Kwa maana nyingine, matukio haya yanatokea karibu na ujio wa pili wa Kristo, lakini baada ya kuanguka nyota, kukiolitokea mwaka 1833 B.K._*
*π
Muhuri sita ulikuwa imeandaa njia kwa ajili ya kazi muhimu ya hawa malaika wanne, na βmalaika apandaye kutoka maawio ya jua.β Kazi yao kuu ni nini?*
_πΌ Tumekwisha kuona na kujifunza katika sura ya nne namna malaika wanavyoongoza mambo ya wanadamu. Hawa βmalaika wanneβ wanafanya kazi katika kila sehemu ya dunia, wakiangalia kazi ya Mungu isiangamizwe._
*πͺοΈ βUpepoβ katika unabii wa Biblia una maana ya migongano, machafuko, na vita kati ya mataifa, vinavyozuia maendeleo ya kazi ya Mungu miongoni mwa wanadamu. (Dan. 7:2; Yer. 25:32) Wote tunafahamu kinachotokea upepo unapovuma kutoka pande nne kwa wakati mmoja. Kimbunga hutokea, nacho huleta uharibifu mkubwa mno.*
_π Yeremia anasimulia kitakachotokea wakati pepo nne za chuki ya wanadamu zitakapofunguliwa: βTazama uovu utatokea toka taifa, na tufani kuu itainuliwa toka pande za mwisho wa dunia, na waliouawa na BWANA siku ile watakuwapo, toka upande mmoja wa dunia hata upande wa pili.β (Yer. 25:32, 33) Hii haiwezeki kuwa kitu kingine isipokuwa vita vya Har-Magedoni vinavyokaribia ambavyo Mungu atawatuma malaika zake kuzuia mpaka amewatia muhuri waaminifu wake._
*π€· Sasa tunajiuliza, muhuri wa Mungu aliye hai ni nini? Ezekieli atatusaidia kuelewa maana yake, kwa maana anataja βalamaβ itakayotolewa katika vipaji vya nyuso za watu wa Mungu. (Eze. 9:3,4). Hii alama ni ishara ya ushindi dhidi ya dhambi na uaminifu wao kwa Bwana.*
_π Kule Misri, malaika aangamizaye alipopita katika nchi kuuawa wazaliwa wote wa kwanza wa Wamisri, βalipita juu ya;β nyumba zilizokuwa na alama ya damu katika vizingiti vya milango. Hivyo katika maangamizi ya mwisho, malaika wangaoamiza wataamriwa, βlakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama.β (Eze. 9:6) βMuhuri wa Mungu,β hivyo ni alama inayowatambulisha kuwa ni watu wa Mungu._
*π K*tiwa katika βvipaji vya nyuso zaoβ huonesha kuwa ni katika tabia. Nguvu inayotia muhuri ni Roho Mtakatifu (Efe. 4:30).*
_π Yohana anaendelea kuelezea muhuri huu katika Ufunuo 14:1 akisema kuwa wale 144,000 wana jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.β Jina la Mungu ni nini? Katika 1 Yohana 4:16, tunasoma: βMungu ni pendo.β Wakati tabia ya watu wa Mungu itakapobadilishwa kuwa upendo kamili, ndipo βjina la Babaβ litakapoandikwa katika vipaji vya nyuso za watu wa Mungu kabla ya malaika wake kuikamilisha historia._
*π Sasa tunajiuliza, Kwa kawaida, ni amri ipi iliyosahauliwe na "wanafunzi" wa Mungu siku hizi? Kwa hakika ni amri nne, amri ya Sabato. Wengi wamegeuka na kuiacha Sabato kweli ya Bwana, ambayo ni siku ya saba, na wamekubali siku ya mapumziko iliyochaguliwa na kuamriwa na Kanisa la Kirumi yaani siku ya kwanza ya juma. Bwana wetu anasema kuwa Roho wake Mtakatifu huwa anawatakasa watu wake wanapoiadhimisha Sabato kwa usahihi.*
> π "Hakika mtazishika sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi(K*t. 31:13),
_β€οΈ Tena ni katika kushika Sabato kwamba watu wa Mungu wanaweza kumfahamu yeye: *"Zitakaseni Sabato zangu; nazo zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu" (Eze. 20:20).*_
*π Pia tusidhanie kuwa Sabato ilikuwa imetolewa kwa ajili ya taifa la Wayahudi peke yao; Mungu alisema kuwa ingekuwa ishara yake na wao katika vizazi vyao vyote milele. K*t. 31: 16, 17). Tangu uumbaji, muda mrefu kabla ya Myahudi ye yote kuwepo, Sabato ilikuwa imetakaswa kwa ajili ya mwanadamu. Yesu kutoka mbinguni aliishika k**a kielelezo chetu.*
_βοΈ Yeye alisema kuwa hakuja kuibadilisha sheria ama kuitangua: *"Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua bali kutimiliza"* *"Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni"* (Mat. 5: 17, 19)_
*π Na zaidi ya hayo, Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuishika Sabato hata baada ya kusulibishwa na kufufuka kwake ( Mat. 24:15-21).*
_βͺ Sabato ya kweli ya siku ya saba ilikuwa inashikwa na mitume na Wakristo wasio Wayahudi (Mdo 18:1, 4; 17: 2; 13:42- 44). Yohana anasema kuwa watu wa Mungu watashika amri zake zote katika iku za mwisho, na hi ni lazima pia iwe pamoja na Sabato: *"hapa ndipo penye subira ya watakatifu ,hao wazishikao amri za Mungu, naimani ya Yesu"* (Ufu. 14: 12)._
*π
Mwisho, Sabato itashikwa kwa dhati katika mbingu na nchi mpya atakazoziumba Bwana (Isa. 66:22, 23). Kupokea "mhuri wa Mungu ni kupokea alama ya itakamtofautisha na kumtenga mtu kutoka kwa wengine kuwa wa pekee kabisa. Malaika waangamizao wanaambiwa, "msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama" (Eze. 9:6).*
_β οΈ Lakini wengine wote, pamoja na "wazee waliokuwa mbele ya nyumba, walikuwa wauawe. ie. kushika Sabato ya kweli kunambainisha mtu kuwa tofauti na watu wengine?_
*β Ndiyo, kwa hakika. Hata katika "kizazi hiki kinachojita cha Kristo; moja ya mambo ya pekee mtu anayoweza kuyashika ni Sabato ya kweli ya Bwana, siku ya saba, ambayo ni Jumamosi. Ulimwengu wote, Wakristo kwa wapagani, mara kwa mara huitumia siku ya Sabato ya kweli ya Bwana k**a siku ya shughuli zao nyingi. Mamilioni, kwa sababu ya mvuto wa kipagani na upapa, wanaitunza siku ya kwanza ya juma badala ya Sabato. Kuishika siku ya saba kwa namna ya pekee ni ushahidi kwamba hakika ndio mhuri wa Mungu aliye hai.*
_πΏ Lakini ni lazima ikumbukwe kwamba kuishika Sabato vyema ni tundala uongofu halisi. Siyo suala tu la kupumzika siku ya Jumamosi. Kupokea mhuri wa Mungu kwa kushika Sabato ya kweli ni kupokea kazi ya Roho Mtakatifu moyoni, "pumziko kutoka katika dhambi na ubinafsi. *"Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe Katika kazi yake, k**a vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake"* (Ebr. 4:9, 10). Hizi "kazi" ni matendo ya kiburi na kujipenda nafsi._
*πΌ Kazi ya malaika huyu ya kuwatia mhuri watu wa Mungu ndiyo muhimu inayotendeka sasa ulimwenguni. Itaendelea kwa "kila a jamii, lugha, na kabila" hadi wafuasi wa kweli wa Mungu waakapokuwa wametiwa mhuri. Hakuna nguvu katika dunia aukuzimu itakayoweza kuzuia kukamilishwa kwa kazi hi.*
_πͺοΈ Kwa kuhusu hili, "Malaka wanne" wanaendelea kuzuia "pepo za vita" katika ulimwengu kwa muda kitambo. Hii inaelezea Mungu anavyoingilia kwa siri shughuli za mataifa yanayopatwa na ukandamizaji uhuru wa dini. Malaika huzuia hizo pepo huku ili kazi ya Inijli iendelee kuhubiriwa._
*β³ Lakini bado muda kidogo - utakuja ule, "wakati wa taabu, mfano wake haukuwepo tangu lilipoanza kuwapo taifa" (Dan. l2:1). Sasa ndiyo wakati wa kupokea. mhuri wa Mungu*
π Mafungu 4-8:
> "Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika b. 1 kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu. Wa kabila Huda kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri. Wa kabila ya Reubeni kmi na mbili elfiu Wa kabila ya Gadi kumi na mbili elfu. Wa kabila Asheri kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Naftali kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Manase kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Simeoni kumi na mbili elfu. Wakabilla ya Lawi kumi na mbili elfu. Wa kabila ya lsakari kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Zabuloni kumi na mbili elfu Wa kabila ya Yhsufu kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Benjamini kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri."
_π Wengine watashangaa vipi Wakristo wagawanywe katika makabli kumi na mawili ya Waisraeli. Tunapata maelezo katika kitabu cha Warumi; "Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa lbrahim yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto Wa ile ahadi wanahesabiwa kuwa wazao (Rum 9:7, 8)._
*π "Maana ye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu.... bali yeye Myahudi aliye Myahudi kwa ndani; na tohara ni ya moyo, andiko: (Rum. 2: 28, 29). Yakobo anaandika waraka wake katika katika roho, si katika Agano jipya kwa jamii ya Wakristo, "kwa kabila kumi na mbili waliotawanyika (Yak1: 1).*
_βͺ Hawa ndio watu wa kweli wa Mungu jamii ya kweli ya Wakristo. Yerusalemu mpya ni mji wa Kristo, lakini malango yake yana majina ya makabila kumi na na wale wote watakaoingia watapitia katika mojawapo ya malango haya. Yesu mwenyewe alikuwa Myahudi kwa ndani, "kwa moyo, katika rohoΖ‘._
*β Kwa nini watu wa Mungu wanagawanywa katika makabila tofauti kumi na mawili? Kila mojawapo ya makabila kumi na mawili ya Waisraeli lilikuwa na tofauti maalumu katika tabia zilizoelezewa otilka Mwa. 49:1-28 na katika K*m. 33:6-24. Siyo hesabu ya wote katika kila kabila wanaohesabiwa katika jumla ya washindi pamoja na 144,000: "Katika kila" kabila walitiwa; muhuri 12,000 pekee.*
*β οΈ Wengine hawakushinda. Msomaji, na tuwe katika wale washindi!*
π Mafungu 9-12:
> "Baada ya hayo nikaona na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa μΈila taifa , na kabila, na jamaa na lugha, wamesimama mbele ya kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao; wakilia kwa sauti kuu wakisema. Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi na Mwana-Kondoo. Na malaika wote walikuwa wakisi mama pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee, na za wale wenye uhai wanne; nao wakaanguka kifulifuli mbele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu. wakisema. Amina; Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uwezo na nguvu zina Mungu wetu hata milele na milele. Amina."
*π Huu "mkutano mkubwa" inawezekana unajumuisha wale l44,000, ambao huenda ni hesabu ya fumbo. Hesabu katika Biblia mara nyingi hazihesabiwi k**a tunavyozihesabu. Yesu alipowalisha Watu 5,000, hesabu hii ilikuwa bila wanawake na watoto, (Mat.14: 1).*
_π Yohana kwanza alisikia "hesabu yao waliotiwa muhuri; na baadaye akaona "mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu; awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, a lugha." Bila shaka huu "mkutano" ni matunda ya mahubiri ya halaika watatu" ambao katika siku za mwisho watapeleka Injili kwa "kila taifa na kabila, na lugha na jamaa" (Ufu. 14:6, 7)._
*π Inawezekana kuwepo mamilioni ya watu! Kuna nafasi yako katika mkutano huo .Wale 144,000 bila shaka ni wale watakaokuwa hai wakati atakapokuja. Watakuwa wamepitia hali maalumu. Wanaweza kuwemo wale waliokuwa wanaishi enzi i za zamani, watakaofufuliwa Bwana atakapokuja (1The 4:16, 17). Tunaambiwa zaidi juu*
π Mafungu 13-17:
> "Akajibu mmoja wa wale wazee akaniambia, Je watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani wametoka wapi? Nikamwambia Bwana wangu, wajua wewe Akaniambia, hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu nao wamefua mavazi yao na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo. Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekal lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao. Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena. wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote. Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai. na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.
*π€ Ni wema wa namna gani kwa mmoja wa wazee ishirini na wanne kutazamia swali letu kutoka kwa Yohana! Mungu anataka tukielewe kitabu hiki!*
_πHii "dhiki ile iliyo kuu", ni sawa na ile iliyozungumziwa Danieli, ambayo itakuja kabla tu ya mwisho: "Wakati huo ( Mlango wa rehema utakapofungwa) Mikaeli atasimama, (kuanza kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile" (Dan. 12:1)._
*β οΈ "Wamepitia wakati wa taabu, mfano uchungu wa wakati wa taabu yake Yakobo (Yer. 30:6, 7); walikuwa Wamestahimili na wamesimama bila Mwokozi wakati wa kumwagwa kwa hukumu mwisho ya Mungu.. Walikuwa wameiona dunia ikidhoofishwa na na maradhi, jua likipewa nguvu kuwaunguza wanadamu kwa joto kali, na wao wenyewe wakiwa wamevumilia mateso, njaa, na kiu.*
_π€οΈ Lakini hawataona njaa tena wala hawatona kiu tena; wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote" (Ufu. 7:16)._
*π₯ Hawa watakuwa wameishi wakati wa mipigo saba ya mwisho (tazama ufunuo 16) bila ya kudhurika.*
_π Hawa ndio wale wanaosemwa katika kitabu cha Zaburi, *"kwa kuwa wewe BWANA ndiwe kimbilio langu; umemfanya Alive juu kuwa makao yako; Mabaya hayatakupata wewe; wala tauni haitaikaribia hema yako. Kwa kuwa amekaza kunipenda. Nitamwokoa; na kumweka juu, kwa kuwa amenijua jina langu."* (Zab. 91:9. 10, 14)._
*π Je, kuna utajiri wo wote ule ambao limwengu huu unaweza kutoa utakaoweza kulingana na nafasi ya kuwemo katika hesabu ya huu "mkutano mkuu"? Tabia iliyojengeka katika maisha haya ndiyo itaamua hali yetu ya baadaye. Kristo atakapokuja, hatabadilisha tabia ya mtu ye yote. Tumepewa muda wa thamani mno ili kuutumia vyema katika kusafisha mavazi yetu ya tabia na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.*
_π’ Kuna machozi mengi katika nyuso zetu sasa; tunafahamu huzuni, msiba, uchungu na dhuluma ya umaskini. Lakini hakutakuwa na machozi tuvaapo mavazi meupe tutakuwa tumejifunza kumtegemea Bwana, na kufahamu kuwa yote aliyokuwa anatufanyia yalikuwa kwa ajili ya manufaa yetu._
*π Kwa nini tulie wakati TUNAJUA KUWA Bwana huyaamuru yote yanayotupata? K**a mama mwenye upendo anayemfariji mtoto wake anayelia, Bwana ameanza kufuta machozi yetu yote hata sasa. Anatufanyia haya sasa tunapopiga magoti mbele zake katika toba ya ombi la siri.*
*π Na atatufanyia yote kwa utimilifu tutakapotembea na Mwana-Kondoo kwenye "Chemchemi za maji yenye uhai.*
Asante kwa kufuatilia somo hili la unabii. Ili kuendelea kupata masomo haya kwa ukamilifu na kufuatilia mfululizo wake, tafadhali tumia viambatanisho vifuatavyo:
π² Whatsapp Channel: Jiunge hapa https://whatsapp.com/channel/0029Vb7hYnB7tkjAYUzMFf01
π Simu: +255754792624
π§ Email: [email protected]
π Karibu tuendelee pamoja kujifunza na kufunuliwa siri za unabii!