13/07/2026
Mmoja wa magwiji wakubwa wa soka atahitimisha taaluma yake bila kushinda taji muhimu zaidi, baada ya mechi ya mwisho ya Kombe la Dunia ya Cristiano Ronaldo akiwa na Ureno kumalizika kwa kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Uhispania katika hatua ya 16 bora.
Mchezaji huyo alibubujikwa na machozi wakati safari yake ya Kombe la Dunia ilipofikia tamati, kufuatia bao la ushindi lililofungwa na Mikel Merino katika muda wa nyongeza, bao lililoiwezesha timu ya nchi jirani kusonga mbele.
Akiwa na umri wa miaka 41, mchezaji huyo ambaye ameshinda tuzo ya Ballon d'Or mara tano, Ligi ya Mabingwa mara tano na Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro) mwaka 2016, amefunga mabao 976 —rekodi ya dunia— akiwa na klabu zake pamoja na timu ya taifa.
Amefunga mabao katika mashindano sita ya Kombe la Dunia, rekodi ya kihistoria.
Hata hivyo, hatua ya karibu zaidi aliyofikia katika mbio zake a kushinda Kombe la Dunia ilikuwa mwaka 2006, wakati Ureno ilipotinga nusu fainali.
Tayari alikuwa ametangaza kuwa hili lingekuwa Kombe lake la Dunia la mwisho, lakini baada ya mechi hiyo alisema: "Nitajadiliana na familia yangu na kufanya maamuzi kwa utulivu," alipoulizwa iwapo ataendelea kuichezea timu yake ya taifa.
Skip content and continue reading
'Nadhani mimi ni mchezaji niliyekamilika zaidi kuwahi kutokea' - Ronaldo7 Februari 2025
Ronaldo na Messi - Ushindani ambao ulitawala soka kwa miongo miwili - lakini nani bora zaidi kati yao?10 Juni 2026
End of content
Mjadala utaendelea kuwa wazi laitiUreno wangekuwa na nafasi nzuri zaidi ya kushinda Kombe hili la Dunia bila shinikizo la kumwanzisha Ronaldo - mchezaji wa klabu ya Al-Nassr - katika kila mechi.