17/12/2025
UJUMBE WA KUPOKEA UDHAMINI – FARNES COMPANY
Kwa heshima na shukrani nyingi, FARNES COMPANY inapenda kutangaza kupokea rasmi udhamini wa MAREFARI unaotolewa katika Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu, kwa lengo la kuboresha maendeleo ya vijana wetu.
Udhamini huu ni ishara ya dhamira ya kweli katika kuunga mkono vijana, kukuza vipaji, elimu, michezo, sanaa na maendeleo ya kijamii kwa ujumla. Kupitia msaada huu, FARNES COMPANY itaendelea kuandaa na kuimarisha programu mbalimbali zitakazowawezesha vijana kujifunza, kujiajiri, na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii yao.
Tunapokea udhamini huu kwa moyo wa shukrani na tunatoa ahadi ya kutumia msaada huu kwa uwazi, uaminifu na kwa malengo yaliyokusudiwa, ili kuleta matokeo chanya na ya kudumu kwa vijana wa Nyarugusu Camp.
Tunamshukuru sana MAREFARI kwa moyo wake wa kujitolea na mshik**ano. Tunaamini ushirikiano huu utaleta mabadiliko makubwa na fursa mpya kwa vijana wetu.
Asanteni sana kwa kuwekeza katika vijana – nguvu ya taifa la kesho.