Upgrade Your Vision, Live Your Destiny

Upgrade Your Vision, Live Your Destiny Heavenly Man,, Son of God, African blood!

24/05/2025

Maisha bila maono ni maisha yasiyo na maana!

Usipotumia uwezo wako ulionao, na kuyasimamia maono yako,

wapo ambao watautumia uwezo wako huo kutimiza maono yao!

Hivo jitahidi kujua, kusudi la kuishi kwako ili utengeneze maono ya uwepo wako duniani

Mafanikio makubwa sio kula, kunywa na kupata Kila kitu, bali mafanikio makubwa ni kuiishi hatima yako uliyopangiwa!
23/05/2025

Mafanikio makubwa sio kula, kunywa na kupata Kila kitu, bali mafanikio makubwa ni kuiishi hatima yako uliyopangiwa!

The most powerful thing ever, in this world is to live your destiny

Kitu Cha maana Sana kwenye Dunia hii ni kuiishi hatima yako,..

Ukipoteza muda kwenye Mambo mengine yasiyokuhusu, baadae utakuja kugundua hakuna Cha maana ulichofanya!

Tafuta Sana kujua kwa nini, ulizaliwa? Na kwanini mpaka Sasa unaishi???

The most powerful thing ever, in this world is to live your destiny Kitu Cha maana Sana kwenye Dunia hii ni kuiishi hati...
23/05/2025

The most powerful thing ever, in this world is to live your destiny

Kitu Cha maana Sana kwenye Dunia hii ni kuiishi hatima yako,..

Ukipoteza muda kwenye Mambo mengine yasiyokuhusu, baadae utakuja kugundua hakuna Cha maana ulichofanya!

Tafuta Sana kujua kwa nini, ulizaliwa? Na kwanini mpaka Sasa unaishi???

Baba anakuita
19/05/2025

Baba anakuita

19/05/2025
12/04/2025

Kinachofanya nchi ya Tanzania isifikie kule inakotakiwa iwe, ni "Mimi kwanza, nchi baadae" hii inapelekea kukosa maono ya nchi..ya Muda mrefu...wakati mwingine hata maono ya muda mfupi hayatimii, kutokana na watu kutanguliza maslahi binafsi...

Mtu akikabidhiwa burungutu la fedha na yeye ndo mwamuzi anahakikisha zinapungua kidogo...piga mfano ...inaanza wizarani inamegwa pesa, kwenye mamlaka husika inamegwa pesa, mpaka ije ifike kwenye mradi..imepungua...kinachofanyika..wanababatiza mradi hivo hivo basi. Umekamilika kwa kiwango dhaifu au, haujakamilika.

Wakati mwingine,,,, mapato kwenye mradi wa nchi ni mengi, lakini vinaingizwa vigharama gharama vya ajabu, ili kumega fungu..Pato linaloenda ni dogo Sana, ndo ukute kiongozi mkuu ni bogas, hakemei Wala kuuliza ,,,,ndo kabisa..Kila siku Pato la nchi hushuka, hasara ya makapuni ya serikali kwenye ripoti ya taifa.

Tunahitaji kuridhika na kuamua kupambania nchi yetu kufika mbali!..na hii inatakiwa ianze na kiongozi mkuu wa nchi..ni mtu mmoja tu, wengine wote watafuata, Yesu alikuwa mmoja tu, wokovu uliingia, Adamu mmoja tu, dhambi iliingia, ni kanuni...tupate wapi mtu jasiri na mwenye hasira ya kuipigania nchi?

Uhusiano wako na Damu ya YESU;Tunafahamu kwamba mtoto kabla hajazaliwa tu, yupo tumboni mwa mama yake, anakuwa na uhusia...
11/04/2025

Uhusiano wako na Damu ya YESU;

Tunafahamu kwamba mtoto kabla hajazaliwa tu, yupo tumboni mwa mama yake, anakuwa na uhusiano wa Moja kwa Moja na baba yake, ndio maana utasikia wanasema tukapime DNA tujue damu hii ni ya nani?

Kwa namna hiyo anagundulika huyu mtoto ni wa fulani, kwa sababu damu ya baba na mwana vinaendana. yaaani damu Moja.

Unapookoka, na kupata kuula mwili wa Kristo na kuinywa Damu yake kwa Imani, tangu hapo unahesabiwa kuwa mtoto wa MUNGU kwa Imani...na hapo mfanano wa wewe na Mungu unaanza kuzaliwa. Unaanza kubadilishwa mwenendo usiofaa wa zamani, na kupata mwenendo mpya ...Yoh 1:12.. Yoh 6:24....

Katika namna yako yote ya kuamini ni muhimu sana kuamini na kukiri kuinywa damu ya Yesu ndiyo inayokupatanisha wewe na baba Mungu, pamoja na Kristo wake.

29/03/2025

JE UMAARUFU NA KUWA NA PESA NYINGI NDO HATIMA??

Kuwa mtu maarufu, au mwenye pesa sio hatima.. Wala maono.

Kuna watu wengi leo wanalia kwa sababu tamaa yao ilikuwa ni pesa, na kweli wakazipata, lakini walipoteza hatima zaoo.. wakabaki kulia na kujutia, kwanini wana pesa na maisha Yana huzuni? Kwanini wana pesa lakini amani haipo? Kwanini wana vitu tele na anaweza kwenda atakako lakini bado, maisha yake ni utumwa na mateso..

Watu wengi huwahisha hatima zao kwa tamaa ya pesa, Hasa vijana wengi Sana, kwa sababu hatima usipoilinda na kuitunza, kwa kudhihirisha kwa ulimwengu kwamba unayo inabaki ndani yako, mpaka atokee mtu wa kukusaidia.. ndio maana watu wengi wamekufa na hatima kubwa Sana za utajiri udumuo na heshima.

Kundi kubwa wanaamini, ukiwa na pesa tu basi ndo Kila kitu, ndio maana utamkuta mhubiri mzuri Sana, ukiangalia ana kusudi la kuhubiri injili ya kweli kimataifa, lakini kwa tamaa ya pesa anadanganyika, anapotoka kwa miujiza feki, uongo na utapeli..baada ya ..miaka kapotea, bila heshima.

Kundi la wasanii vilevile wanadanganyika mtu ni mwimbaji mzuri ukiangalia huyu atafika mbali lakini kwa tamaa ya pesa anaingia kwenye kutaka pesa za chapu, mikataba freemason, kwa waganga.. .kweli wanampa madawa ya masharti anavuma na kutamba na vipesa na magari ya kifahari baada ya muda amepotea

Nikukumbushe watu walioishi hatima zao, Ev. Kulola, Baba Lola, Bonke, Kenneth hageni, Benson Idahosa, wasanii Remi ongala, na wengine wengi...unaona wamedumu katika hatima zao, zimewaletea utajiri na heshima.

Haina maana pesa ni mbaya Ila tafuta pesa ndani ya kusudi la kuletwa kwako duniani, unaupata utajiri wenye heshima na utukufu kwa Mungu.

28/03/2025

Uwe na maono, nenda hatua kwa hatua kuyafikia, usitake kuwa na hatua ya juu kwa mara Moja, utaanguka.

Kwani kwa kawaida unapoanza na hatua ya Chini, unatengeneza msingi mzuri wa maono yako!

28/03/2025

Maono na hatima hutimilizwa vema kwa kuwaheshimu watu!.

27/03/2025

Unapopewa nafasi onesha uwezo wako, huo utakupa kukubalika na watu zaidi kuliko kujipendekeza

Address

Dodoma
Kongwa

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Upgrade Your Vision, Live Your Destiny posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category