yegowasutelevision

Website

yegowasutelevision kutoa habari za uhakika Kila zinapochipuka

JESHI LA POLISI MKOA WA MARA LINAMSHIKILIA KENETH NKIKO KWA TUHUMA ZA MAUAJI.Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia ...
06/10/2026

JESHI LA POLISI MKOA WA MARA LINAMSHIKILIA KENETH NKIKO KWA TUHUMA ZA MAUAJI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Keneth Roja Nkiko, mwenye umri wa miaka 28, mkazi wa Mwigobero, kwa tuhuma za kumuua Magreth Hamisi Richard, mwenye umri wa miaka 22, mfanyabiashara na mkazi wa Mukendo, Halmashauri ya Manispaa ya Musoma.

Tukio hilo limetokea tarehe 05 Oktoba 2026, majira ya saa 4.00 asubuhi, katika Mtaa wa Mwigobero B, Kata ya Mwigobero, Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, Mkoa wa Mara.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alimshambulia marehemu kwa kumpiga kichwani kwa kutumia kitu butu, na baadaye kumchoma kwa kitu chenye ncha kali katika sehemu mbalimbali za mwili. Kutokana na majeraha aliyoyapata, marehemu alipoteza maisha.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi kwani mtuhumiwa alipata taarifa kuwa mpenzi wake anamsaliti kwa kuingiza wanaume wengine ndani wakati yeye akiwa hayupo.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara linatoa wito kwa wananchi kutokujichukulia sheria mkononi pindi wanapokumbana na migogoro ya kimapenzi au ya kifamilia. Wananchi wanashauriwa kutumia njia za kisheria na taasisi husika za kijamii kutatua migogoro hiyo, badala ya kutumia nguvu au kufanya vitendo vinavyoweza kusababisha madhara au kupoteza maisha.

Share on Whatsapp :

ENDELEA KUFUATILIA MATANGAZO YETU USISAHAU KU SUBSCRIBE SHARE NA COMMENT 👇
30/09/2026

ENDELEA KUFUATILIA MATANGAZO YETU USISAHAU KU SUBSCRIBE SHARE NA COMMENT 👇

...Endelea kufuatilia habari zetu kupitia mitandao ya kijamii. Face...

HATIMA YA MADEREVA NCHINI BAADA YA MGOMO KUANZIA SIKU JANA
30/09/2026

HATIMA YA MADEREVA NCHINI BAADA YA MGOMO KUANZIA SIKU JANA

...Endelea kufuatilia habari zetu kupitia mitandao ya kijamii. Face...

29/09/2026
29/09/2026

MGOMO WA MABASI WATINGISHA MARA: MADEREVA WALALAMIKA, ABIRIA WAKWAMA — POLISI WATOA TAMKO

Mgomo wa mabasi na magari ya abiria umeendelea kuchukua sura mpya nchini, huku baadhi ya madereva wakieleza malalamiko yao kuhusu utekelezaji wa sheria za barabarani, mfumo wa pointi, kufungiwa leseni na taratibu za mafunzo, wakati abiria na wafanyabiashara wadogo wakieleza namna hali hiyo ilivyowaathiri katika Kituo Kikuu cha Mabasi ya Mikoani Bweri mkoani Mara.

Hali hiyo imeonekana katika kituo hicho ambapo baadhi ya abiria wamekwama kwa muda mrefu wakisubiri usafiri, huku wengine wakisema hawakuwa na uhakika wa muda ambao safari zao zingeanza.

Kwa upande wa madereva, malalamiko makubwa yameelekezwa kwenye mfumo wa pointi za makosa ya barabarani, faini, kufungiwa leseni pamoja na kile wanachokieleza kuwa ni ukaguzi wa mara kwa mara katika vituo mbalimbali vya barabarani.

Dereva Ramadhani Juma, anayefanya safari kati ya Mara, Musoma na Iringa, amesema madereva wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali wanapotekeleza majukumu yao.

“Sisi madereva tuna tatizo la kunyanyaswa na traffic barabarani. Unapokuwa umeendesha vizuri, unafika sehemu traffic anaweza kukuandikia faini na kukukatia pointi. Wakati mwingine leseni yako inaweza kufungiwa miezi mitatu au miezi sita.”

Ramadhani amesema kufungiwa leseni kunaathiri maisha ya dereva pamoja na familia yake, kwa kuwa kazi ya udereva ndiyo chanzo cha kipato.

“Kwa serikali tunaomba watusikilize sisi madereva, kwa jinsi tunavyofanya kazi na changamoto tunazopitia barabarani. Kwanza miundombinu, barabara ni mbovu. Tunaomba serikali itusikilize.”

Amesema pia madereva hukutana na ukaguzi katika maeneo mbalimbali, jambo ambalo amesema wakati mwingine hupelekea dereva kukutana na makosa tofauti katika safari moja.

“Unafika sehemu moja unakaguliwa, unatoka hapo unakaguliwa tena. Barabara ya kilomita hamsini unakuta kuna vituo vingi vya ukaguzi. Kila mmoja anakagua na anaona uko salama, lakini unafika sehemu nyingine unaandikiwa kosa.”

Ramadhani pia amesema baadhi ya madereva hufanya kazi bila mikataba rasmi ya ajira, hali ambayo amesema ni changamoto nyingine inayowakabili.

“Mimi ni dereva wa basi. Sina mkataba. Ukienda kuomba mkataba kwa mwajiri wako anaweza kukuambia gari yangu nenda pale. Hilo linakuwa changamoto.”

Dereva mwingine amesema kero nyingine inayowakabili madereva ni taratibu za mafunzo na mitihani, akieleza kuwa baadhi yao hulazimika kusoma tena kwa kila daraja la leseni licha ya kuwa tayari wana uzoefu wa kuendesha.

“Kero ya madereva ambayo inatusumbua hasa, kwa upande wangu cha kwanza ninaona LATRA. Wamepandisha gharama nyingi, lakini bado inakuwa kwamba dereva unaambiwa ukafanye mtihani LATRA.”

Amehoji ulazima wa dereva ambaye tayari amesomea udereva na ana uzoefu kuendelea kutakiwa kusoma kila daraja.

“Dereva huyu alishasoma na ana uzoefu mwingi. Unaambiwa kila daraja ukalisome. Dereva ni yuleyule, haubadiliki. Lakini unaambiwa kila daraja ukalisome. Hiyo ni kero kubwa.”

Aidha, amesema kuna mkanganyiko kwa baadhi ya madereva kuhusu nyaraka zinazotakiwa wakati wa ukaguzi, hasa kati ya leseni na vyeti vingine vya mafunzo au uhakiki.

“Leo dereva amesoma, una cheti, una leseni, unaambiwa cheti cha uhakiki. Sasa hapo polisi watuambie kati ya cheti cha uhakiki na leseni tutembee na vitu gani vya uhakika ambavyo wao wanaviamini.”

Wakati madereva wakieleza changamoto zao, abiria wamejikuta wakisubiri kwa muda mrefu katika Kituo cha Mabasi Bweri.

Elisha, mmoja wa abiria waliokwama, amesema amefika kituoni hapo tangu asubuhi akiwa na safari ya Mwanza lakini hadi muda huo hakuwa na uhakika wa muda wa kuondoka.

“Nimefika hapa tangu asubuhi. Gharama pia zinanishinda, mpaka sasa hivi niko hapa hata chai sijanywa. Sijui nitalala wapi, sijui nitafanya nini. Natamani tu iwezekane magari yausafiri ili tuondoke, tuende tunakokwenda.”

Naye Estericia, ambaye alikuwa na safari ya Mwanza, amesema awali hakufahamu kuhusu mgomo huo na alishangazwa baada ya kufika kituoni na kukuta hali tofauti na matarajio yake.

“Nikauliza, nikaambiwa kuna mgomo. Nikasema mgomo wa nini? Nikaambiwa ni kwa sababu ya usumbufu wanaofanyiwa madereva na makosa madogo madogo. Mimi nikashangaa.”

Amesema alipewa taarifa kuwa gari lingeondoka saa nne, lakini muda ulipita bila safari kuanza.

“Nikauliza saa ngapi? Nikaambiwa anatoka saa nne... lakini hadi sasa bado. Mimi nina safari inaenda Mwanza.”

Mgomo huo pia umeathiri wafanyabiashara wadogo wanaotegemea vituo vya mabasi kupata wateja.

Mariamu Mwoni, mmoja wa wafanyabiashara katika kituo hicho, amesema biashara yake imeathirika kutokana na kusimama kwa baadhi ya safari.

“Mimi k**a mjasiriamali wa Bweri Standi, kwa kweli mgomo huu wa madereva umeleta shida kubwa. Hata mimi k**a mjasiriamali mdogo ninayetembeza bidhaa kwenye magari ili nipate kuishi, kweli umeniazi.”

Ameomba serikali na madereva kufikia mwafaka ili mgomo huo umalizike.

“Tunaomba mfanye marekebisho kati yenu na serikali pamoja na madereva. Kwa kweli huu mgomo uishe kwa sababu umetuathiri. Sisi tumetoka nyumbani kutafuta watoto katika biashara hizi.”

Naye Maria Fili, ambaye ni mjasiriamali mwingine mdogo, amesema wamekuwa wakizunguka kituoni bila kupata magari ya kusafiri.

“Kwa mgomo huu hata sisi wajasiriamali wadogo tumeumia. Tumesimama tu hivi hivi na bidhaa zetu, hatujui twende wapi. Kila mstari tunaenda tunakuta hakuna gari.”

Ameomba hatua zichukuliwe ili huduma ya usafiri irejee.

Abiria mwingine, Mwalimu Daktari Hospitalis kutoka Buturi, amesema changamoto imekuwa kubwa kwa baadhi ya wasafiri ambao walitoka maeneo yao wakiamini kuwa safari zingeendelea k**a kawaida.

Amesema baadhi yao walifikishwa katika kituo hicho, lakini walipofika wakakutana na mgomo na kukosa usafiri wa kuendelea na safari zao.

“Tumefika hapa, tumepata tatizo. Changamoto ni kwamba madereva wamegoma. Tatizo la msingi ni sisi tuna changamoto ya usafirishaji. Tunahitaji usafiri na hawa wamegoma.”

KWA UPANDE WA JESHI LA POLISI MKOANI MARA LIMESEMA HUO NI UVUMI WA MITANDAO KWA MARA HUDUMA YA USAFIRI INAENDELEA K**A KAWAIDA.

Akizungumzia hali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, SACP Pius Lutumo, amesema taarifa zilizokuwa zikisambaa kwenye mitandao zilisababisha baadhi ya madereva kuwa na hofu na kusita kufanya safari zao za kawaida.

Hata hivyo, amesema kwa Mkoa wa Mara, hususan Musoma, kampuni nyingi zimeendelea na safari zao k**a kawaida na Jeshi la Polisi limekuwa likifuatilia usalama wa magari yanayosafiri.

“Kwa hapa Mara na Musoma, baadhi ya madereva walipata hofu asubuhi, lakini wengine wameanza safari zao k**a kawaida. Kampuni nyingi zimefanya safari zao k**a kawaida, na hao waliofanya safari zao tumeendelea kuwafuatilia njia yote na hawajapata shida yoyote.”

SACP Lutumo amesema Jeshi la Polisi linaendelea kufanya doria katika barabara kuu kutoka Musoma kuelekea Mwanza na kuwasiliana na mikoa inayounganisha njia hiyo, ikiwemo Simiyu na Shinyanga.

“Tumewaambia, hofu hiyo ilikuwepo waendelee. Na sisi tuko barabarani tunafanya doria. Njia yote hii kutoka Musoma kwenda Mwanza tunawasiliana na Simiyu, Shinyanga. Barabara ni nzuri, magari ya polisi yapo yanafanya doria. Kwa hiyo hali ni salama, watu wasitie ile hofu ambayo haina msingi.”

Amesema vituo vya mabasi vina taratibu zake za kawaida za kupanga magari yanayoanza safari na yanayofuata, hivyo wananchi wasichukulie kila hali ya kusubiri kuwa ni ishara ya kutokuwa salama.

Aidha, amesema Jeshi la Polisi linafahamu kuwa katika mazingira k**a hayo kunaweza kutokea taarifa za upotoshaji au propaganda zinazoweza kuwatia hofu wananchi.

“Tunatambua kwenye mambo k**a haya kuna kuwa na propaganda. Tunafahamu wapo vijana ambao wamepandikizwa kufanya propaganda. Lakini hali halisi tunaiona barabarani. Hali halisi tunaona watu wanapanda magari, wanatembea.”

Kamanda huyo amewataka wananchi kupuuza taarifa ambazo hazina msingi na kuendelea kufuata taarifa rasmi.

“Watu ambao wanatoa propaganda nasema tuzipuuze, kwa sababu ni watu ambao wamepandikizwa kwa ajili ya kusababisha mtu mwingine asitoe gari lake akiamini kwamba hali ni mbaya. Kwa hiyo tupuuze vitu k**a hivyo.”

SACP Lutumo pia amesema mtu yeyote atakayebainika kuwazuia watu wanaofuata sheria na taratibu atachukuliwa hatua.

“Tunaendelea kutekeleza wajibu wetu wa kufanya doria highway, na mtu yeyote atakayeonekana kuzuia watu wanaofuata sheria atachukuliwa hatua kali. Hatutakuwa na muhali dhidi ya mtu ambaye atasubutu kuzuia watu wanaofuata sheria na taratibu.”

Kwa upande wa abiria na wafanyabiashara, matarajio yao ni kuona pande zinazohusika zikifikia mwafaka ili huduma ya usafiri irejee kikamilifu na wananchi waendelee na shughuli zao za kila siku.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara limesema litaendelea na doria na ufuatiliaji wa hali ya usalama barabarani, huku likiwataka wasafiri na kampuni za usafirishaji kuendelea na safari kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.

25/09/2026

...Endelea kufuatilia habari zetu kupitia mitandao ya kijamii. Face...

WANANCHI NAGUSI WAPATIWA ELIMU YA USALAMA NA TAHADHARI ZA EL NIÑOWananchi wa Kata ya Nagusi, Tarafa ya Grumet, Wilaya ya...
25/09/2026

WANANCHI NAGUSI WAPATIWA ELIMU YA USALAMA NA TAHADHARI ZA EL NIÑO

Wananchi wa Kata ya Nagusi, Tarafa ya Grumet, Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, wamepatiwa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya usalama na ustawi wa jamii, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Jeshi la Polisi za kuendelea kushirikiana na wananchi katika kuimarisha ulinzi na usalama katika jamii.

Elimu hiyo imetolewa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (A/INSP) Kubeleka, ambapo wananchi wameelimishwa kuhusu umuhimu wa usafi wa mazingira, kuchukua tahadhari dhidi ya mvua za El Niño pamoja na kujiandaa kwa kuweka akiba ya chakula ili kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza.

Aidha, A/INSP Kubeleka ametoa elimu kuhusu namna ya kujikinga na wizi wa kimtandao pamoja na umuhimu wa wazazi kuwajibika katika malezi bora ya watoto. Wananchi wamehimizwa kuwa sehemu ya ulinzi wa jamii kwa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi, kutoa taarifa kwa wakati kuhusu vitendo vya uhalifu na matukio yanayoweza kuhatarisha usalama, kwani usalama wa jamii ni jukumu la pamoja linalohitaji ushirikiano wa karibu kati ya Jeshi la Polisi na wananchi.

24/09/2026

11 MBARONI KWA KUSABABISHA KIFO CHA BODABODA -MARA

MUWASA YAOMBA RADHI WANANCHI , HUDUMA YA MAJI YAANZA KUREJEA BAADA YA CHANGAMOTO YA VIFAAMUSOMA — Mamlaka ya Majisafi na...
24/09/2026

MUWASA YAOMBA RADHI WANANCHI , HUDUMA YA MAJI YAANZA KUREJEA BAADA YA CHANGAMOTO YA VIFAA
MUSOMA — Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) imewaomba radhi wakazi wa Manispaa ya Musoma walioathirika na changamoto ya upatikanaji wa maji iliyodumu kwa zaidi ya mwezi mmoja, huku ikieleza kuwa huduma ya maji imeanza kurejea baada ya hatua zilizochukuliwa kurekebisha hitilafu ya kiufundi.

Mkurugenzi Mtendaji wa MUWASA, Bi. Esther Gilyoma, amesema changamoto hiyo ilisababishwa na kuharibika kwa kifaa muhimu katika mfumo wa uzalishaji na usambazaji wa maji kinachojulikana k**a Variable Frequency Drive (VFD).

Amesema maeneo ya miinuko ndiyo yaliyoathirika zaidi, hali iliyosababisha baadhi ya wananchi kukosa huduma ya maji na kuibua malalamiko mbalimbali.

Bi. Gilyoma amesema MUWASA inatambua usumbufu ambao wananchi wameupata na hivyo imeomba radhi kwa wananchi wote walioathirika.

Amesema, hata hivyo, changamoto hiyo haikutokana na mamlaka kutotaka kuwahudumia wananchi, bali ilitokana na hitilafu ya kiufundi iliyokuwa nje ya uwezo wa mamlaka.

Katika kukabiliana na hali hiyo, MUWASA ililazimika kufanya mgao wa maji ili kuhakikisha maeneo mengine yanaendelea kupata huduma wakati ikitafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.

Kwa sasa, amesema, hatua mbalimbali zimechukuliwa na huduma ya maji imeanza kurejea, huku mamlaka ikiendelea kufuatilia mfumo wa uzalishaji na usambazaji ili kuhakikisha huduma inaimarika zaidi.

Mamlaka pia imepata msaada kutoka Wizara ya Maji , ambapo kifaa hicho kilichosaidia kurejesha uzalishaji tayari kimefungwa.

Aidha, kifaa kingine ambacho MUWASA ilikuwa imeagiza kutoka India tayari kimewasili na kiko tayari kwa ajili ya kufanyiwa majaribio.

MUWASA imesema mahitaji ya maji katika Manispaa ya Musoma yanafikia takribani lita milioni thelathini (30 milioni) kwa siku, huku uwezo wa uzalishaji nao lita milioni thelathini na mbili kwa siku.

Mamlaka imesema inaendelea kusimamia mitambo na miundombinu yake ili kuhakikisha uzalishaji unaendelea katika kiwango hicho na wananchi wanaendelea kupata huduma kwa uhakika.

MUWASA pia imeeleza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Maji imeendelea kuwekeza fedha katika kuboresha huduma ya maji Musoma, ikiwemo mradi mkubwa wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 11 ambao umefikia takribani asilimia 90 ya utekelezaji.

Mradi huo unahudumia maeneo yenye idadi kubwa ya wananchi, ukiwemo Bisumwa, nyankanga ,ziroziro na Mmazami wilaya ya Butiama, huku miundombinu ya mabomba ikiendelea kusambazwa.

Mradi huo umefika pia hadi Mazami, hatua inayolenga kuongeza uwezo wa upatikanaji na usambazaji wa maji katika Manispaa ya Musoma.

MUWASA imesema miradi mingine pia inaendelea katika maeneo ambayo bado hayajafikiwa kikamilifu na huduma, ikiwemo baadhi ya maeneo ya pembezoni k**a .

Kuhusu mfumo wa mita za malipo kabla, MUWASA imesema imeanza kuutekeleza na tayari imefunga takribani mita 500, huku ikiendelea kutoa elimu kwa wananchi.

Mamlaka inaendelea kutafuta ushirikiano na wadau mbalimbali ili kupata mita zaidi na kuzisambaza katika maeneo mengi.

Lengo ni kupunguza changamoto na malalamiko yanayoweza kujitokeza katika mfumo wa malipo baada ya matumizi.

MUWASA pia imesema imepokea maelekezo kutoka Serikali, uongozi wa Mkoa na Wizara ya Maji ya kujiandaa kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa msimu wa mvua.

Mamlaka imejipanga kuhakikisha dawa za kutibu maji zinapatikana kwa kiwango cha kutosha, kwa kuwa mvua zinaweza kusababisha mabadiliko katika hali na ubora wa maji kwenye vyanzo.

Aidha, inaendelea kuimarisha miundombinu ya maji na kuhakikisha mabomba yanafika katika maeneo yaliyolengwa.

Bi. Gilyoma amesisitiza kuwa MUWASA itaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali kuhakikisha wakazi wa Manispaa ya Musoma na maeneo ya pembezoni wanapata huduma ya maji kwa wakati.

Pia amewataka wananchi kutunza miundombinu ya maji iliyowezeshwa na Serikali, akieleza kuwa ulinzi wa miundombinu hiyo ni muhimu kwa ajili ya kuhakikisha huduma inaendelea kupatikana sasa na kwa vizazi vijavyo.

MUWASA imesema inaendelea kufuatilia hali ya huduma baada ya kurejea kwa uzalishaji, huku ikisisitiza dhamira yake ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji kwa uhakika.

Maji ni uhai hayana tajiri wala maskini— na kwa sasa, huduma imeanza kurejea katika maeneo yaliyoathirika.

Address

Musoma
Musoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when yegowasutelevision posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category