Kigoma Yetu DamDam

Kigoma Yetu DamDam Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Kigoma Yetu DamDam, Real Estate, Kigoma Manispaa, Kafr al-Dawar.

Mwenyekiti wa Taifa wa  ACT-Wazalendo, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema, Chama hicho ndicho pekee kilichobeba ma...
29/09/2024

Mwenyekiti wa Taifa wa ACT-Wazalendo, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema, Chama hicho ndicho pekee kilichobeba matumaini ya Umma wa Wazanzibari, na ndiyo maana Mikutano na Vikao vivavyoendelea sasa kote Nchini, vimechukua taswira ya kutatua changamoto za wananchi wote, ikiwa ni sehemu ya Mwongozo na Ahadi yao ya 'The Brand Promise'

Mheshimiwa Othman, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameyasema hayo leo Septemba 29, 2024 alipokutana na kufanya mazungumzo na Wazee wa Mkoa wa Kichama wa Mkoani, huko Chole Kengeja, Mkoa wa Kusni Pemba, ikiwa ni Sehemu ya kusikiliza na kutatua changamoto zao, pamoja na kubadilishana mawazo.

Amesema, Chama hicho kinaelewa kwamba Umma wa Wananchi, kwa sasa unakabiliwa na wimbi la changamoto, zikiwemo za adha na ugumu wa maisha, bali Sera za Chama hicho katu haziwezi kuwasaliti, na Viongozi wataendekelea kuwafikia mara kwa mara kwa lengo la kuzitatua na kukabiliana nazo.

"Sisi tunaelewa kwamba sasa Wananchi wameelemewa na shida na matatizo; na pia zipo hila na njama nyingi ovu za watawala za kuwatoa Wananchi katika imani kuelekea Uchaguzi wa Oktoba 2025, bali la msingi ni kusimamia dhamira ya dhati ya Chama chetu ya kuleta Ukombozi na Mamlaka Kamili ya Visiwa hivi", amesema Mheshimiwa Othman.

Naye, Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho upande wa Zanzibar, Ndugu Ismail Jussa amesema, "zama za kudanganyana na kuwajengea hofu Wananchi zimeisha, sasa ni muda wa uwazi, na katika yote haya CCM hawana manusura kwani msingi wa harakati hizi una mizizi mikubwa na upo nyoyoni mwetu",

Jussa amewahimiza Wazee hao kuwa dira njema kwa jamii zao, ili Vijana nao wafuate Kigezo cha kuipigania Heshima ya Nchi hii.

Kikao hicho ambacho kimefanyika katika Ukumbi wa Judo, uliopo Chole, Shehia ya Kengeja, Jimbo la Mtambile Mkoa wa Kusini Pemba, kimewajumuisha pia Wazee wa Chama, Wazee wa Mji, Watu Mashuhuri, Masheikh pamoja na Viongozi mbali mbali, wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa ACT- Wazalendo Zanzibar, Omar Ali Shehe.

Mheshimiwa Othman ambaye yupo kisiwani Pemba kwa ziara maalum inayojumuisha shughuli za Kisiasa, Serikali na kijamii, akiwa ameambatana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib, jioni ya leo atahutubia Mkutano wa Hadhana katika jimbo Chambani pia Mkoa wa Kusini Pemba.

Kitengo cha Habari
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Septemba 29, 2024.

"SITAOMBA RADHI, CUF INAKUFA KWELI"-ADO"Nimesoma tamko la CUF kunitaka kuomba radhi kwa kauli yangu kuwa CUF inakufa na ...
18/09/2024

"SITAOMBA RADHI, CUF INAKUFA KWELI"-ADO

"Nimesoma tamko la CUF kunitaka kuomba radhi kwa kauli yangu kuwa CUF inakufa na kuwataka wanachama na viongozi wake waliosalia ambao wana moyo wa mapambano kujiunga na ACT Wazalendo. Msimamo wangu ni kuwa sitaomba radhi kwa kauli yangu"- Ado

"Kazi ya siasa ni kazi ya ushawishi. Ushawishi unafanywa kwa hoja sio matusi wala vitisho. Tamko la CUF lililotolewa na Mkurugenzi wake wa Habari ni ishara ya wazi ya Taasisi inayokata roho. Hakuna Taasisi makini ingeruhusu tamko lililosheheni matusi k**a lile litoke kwa umma"-Ado

"Binafsi sitaacha kuwashawishi wanachama wa CUF kuja ACT Wazalendo k**a ambavyo ninafanya kwa wanachama wa CCM, Chadema, wasio na vyama nk. Hiyo ndio kazi ya mwanasiasa. Badala ya kutoa matusi na vitisho, CUF pia wana wajibu wa kufanya hivyo" Ado

"Ninarejea ujumbe wangu kwa wanachama na viongozi wote wa CUF wenye nia ya dhati ya kuendeleza mapambano ya kupigania demokrasia: CUF INAKATA ROHO, KARIBUNI ACT WAZALENDO" Ado

16/09/2024

Wanawake wanachekesha kweli, anataka Mwanaume mwenye pesa wakati yeye mwenyewe kapuku!!😁😁😁

16/09/2024

Wakikuuliza ...
Mbona Siku Hizo upo kimnya sana,Waambie kipindi Kile cha Zamani Nilikuwa Sijui Kutofautisha Kati ya Marafiki Na Wanafiki

Ameandika KC Mikoa 17/39 imekamilisha kuchagua viongozi wao wa mikoa wa  2024-20291. Tanga2. Morogoro 3. Kaskazini A4. W...
15/01/2024

Ameandika KC

Mikoa 17/39 imekamilisha kuchagua viongozi wao wa mikoa wa 2024-2029

1. Tanga
2. Morogoro
3. Kaskazini A
4. Wete
5. Kigoma
6. Kilimanjaro
7. Iringa
8. Njombe
9. Magharibi A
10. ChakeChake
11. Mkoani
12. Kagera
13. Geita
14. Tabora
15. Ruvuma
16. Arusha
17. Njombe

Leo 15/01/2024 mikoa ya

1. Mbeya
2. Singida
3. Mara
4. Selous
inakamilisha chaguzi zake.

Nawapongeza sana Wanachama wote wa ACT Wazalendo kwa kasi hii kubwa ya Ujenzi wa Chama chetu.

Nawatakia Uchaguzi mwema Wanachama wa Mikoa yote iliyobakia.

KARIBU MAGICIAN "Black Messi" 🦍💪Tumefanikiwa kumsajili winga hatari Nyenyezi Juma  kutoka Inter Star ya nchini Burundi.H...
01/01/2024

KARIBU MAGICIAN "Black Messi" 🦍💪

Tumefanikiwa kumsajili winga hatari Nyenyezi Juma kutoka Inter Star ya nchini Burundi.

Huyu sio tu winga bali ni Burudani, Mtafurahi Watanganyika.

Karibu fundi wa boli

Nb: Endelea kutazama vipindi vinavyofuata kutoka hapahapa kwa Watanganyika📺😇


MAAZIMIO YA KAMATI KUU YA CHAMA CHA ACT WAZALENDOTarehe 20 Desemba 2023, Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo ilifanya ...
21/12/2023

MAAZIMIO YA KAMATI KUU YA CHAMA CHA ACT WAZALENDO

Tarehe 20 Desemba 2023, Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo ilifanya kikao chake cha kawaida katika Ukumbi wa Juma Duni Haji uliopo katika Ofisi ya Makao Makuu ya Chama, Dar es salaam.

Pamoja na mambo mengine, Kamati Kuu ya Chama ilipokea Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Chama wa Mwaka 2023, kufanya tathmini ya kina ya utekelezaji wake na kupanga vipaumbele vya Chama kwa mwaka 2024.

Kamati Kuu ilipokea pia Taarifa ya Sekretarieti juu ya hali ya kisiasa nchini na kutoka na maelekezo mahsusi.

Baada ya mjadala wa kina juu ya ajenda zilizowasilishwa, Kamati Kuu iliazimia ifuatavyo;-

1. Uchaguzi wa Ndani ya Chama:

Kamati Kuu ya Chama imeipongeza Sekretarieti ya Chama Taifa na viongozi wa Mikoa, Majimbo, Kata na Matawi kwa mafanikio makubwa ambayo Chama kimeyapata kwenye Programu ya Uchaguzi wa Ndani ya Chama inayoendelea kutekelezwa. Mafanikio yaliyopatikana kwenye uchaguzi wa ndani ya Chama yamedhihirisha kuwa ACT Wazalendo ni chama kinachokua kwa kasi zaidi nchini na chenye taswira ya kitaifa.

Kati ya majimbo 264 yaliyopo nchini, Majimbo 260 yameshakamilisha uchaguzi sawa na 98.5%. Kwa upande wa Zanzibar, Majimbo yote 50 yameshafanya uchaguzi, sawa na 100%. Kwa upande wa Bara, kati ya majimbo 214, majimbo 210 yamefanya uchaguzi sawa na 98%. Majimbo 4 ambayo hayajafanya uchaguzi ni Kibakwe (Dodoma), Manyoni Magharibi (Singida), Mufindi Kusini (Iringa) na Hanang (Manyara).

Chaguzi za majimbo haya, isipokuwa jimbo la Hanang ambalo limekumbwa na janga la mafuriko ya tope, zinatarajiwa kukamilishwa ndani ya mwezi Desemba 2023. Uchaguzi wa Jimbo la Hanang utafanyika baada ya tathmini ya urejeshwaji wa hali ya kawaida ya maisha ya wananchi wa Hanang.

Kwa upande wa chaguzi za Mikoa, Kamati Kuu ya Chama Taifa imeazimia kuwa chaguzi hizo zifanyike kuanzia tarehe 12 Januari hadi 21 Januari 2023.

2. Mkutano Mkuu wa Chama Taifa:

Ili kutekeleza agizo la Halmashauri Kuu ya Chama Taifa iliyoagiza Mkutano Mkuu wa Chama Taifa ufanyike Mwezi Machi 2024, Kamati Kuu ya Chama Taifa imepanga Mkutano Mkuu ufanyike kwa siku mbili, tarehe 2 Machi hadi 3 Machi 2024.

Pamoja na mambo mengine, Mkutano Mkuu Taifa utafanya uchaguzi wa viongozi wa Chama wa Kitaifa na kufanya mabadiliko ya Katiba ya Chama.

Kamati Kuu ya Chama Taifa imeagiza Sekretarieti ya Chama kuhakikisha kuwa, k**a ilivyo ada, wanachama wanashirikishwa ipasavyo katika kuchangia gharama za Mkutano Mkuu wa Chama.

3. Mabadiliko ya Katiba ya Chama:

Kamati Kuu ya Chama imeridhia hoja iliyowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Chama ya kufanya mabadiliko ya 4 ya Katiba ya ACT Wazalendo Toleo la Mwaka 2015 ili kuboresha muundo na ufanisi wa Chama.

Kamati Kuu imeelekeza mchakato wa kukusanya maoni juu ya mabadiliko ya Katiba ya Chama kutoka kwa wanachama na viongozi wa ngazi zote uanze mara moja.

Kamati Kuu imeagiza Sekretarieti pia kuandaa rasimu ya Sera ya Jinsia na Ushirikishwaji wa Makundi Maalum na Sera ya Vijana kwa ajili ya kuchochea ushiriki mpana zaidi wa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika vyombo vya maamuzi vya Chama.

4. Mageuzi ya Kisiasa Nchini:

Kamati Kuu ilipokea Taarifa ya Hali ya Siasa Nchini ambayo pamoja na mambo mengine ilifanya uchambuzi wa kina wa miswada mitatu (Muswada wa Tume ya Uchaguzi, Muswada wa Uchaguzi na Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa) iliyowasilishwa Bungeni na Serikali na kusomwa kwa mara ya kwanza tarehe 10 Novemba 2023.

Kamati Kuu ya Chama imebaini kuwa miswada hiyo bado ina mapungufu makubwa na kwa sehemu kubwa haiakisi mapendekezo ya wadau wa demokrasia yanayopatikana kwenye Taarifa ya Kikosi Kazi cha Wadau wa Demokrasia kilichoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Kamati Kuu imeainisha masuala 10 ya kipaumbele ambayo ni lazima yafanyiwe maboresho kwenye miswada hiyo. Kamati Kuu imebainisha kuwa iwapo maeneo haya hayatafanyiwa kazi, miswada hiyo itapoteza maana yake na kuiathiri falsafa ya ‘4R’ ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan iliyokusudia kufungua ukurasa mpya wa kisiasa nchini.

Maeneo husika ni k**a ifuatavyo;-

i) Tume Huru ya Uchaguzi kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu;

ii) Tume ya Uchaguzi kuwa na watendaji wake watakaosimamia uchaguzi badala ya Wakurugenzi wa Halmashauri;

iii) Viongozi wakuu wote wa Tume (Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Makamishna na Mkurugenzi wa Uchaguzi) wapatikane kwa kufanyiwa usaili na Kamati ya Usaili kabla ya kuteuliwa na Mh. Rais.

iv) Kuboresha muundo wa Tume ya Uchaguzi kulingana na maoni ya wadau wa Demokrasia ili kuihakikishia uhuru wake ikiwemo wajumbe wa Tume kutoondolewa ofisini kwa urahisi (security of tenure);

v) Kuboresha Kamati ya Uteuzi kulingana na mapendekezo ya Kikosi Kazi;

vi) Kuweka utaratibu mpya wa ruzuku kulingana na mapendekezo ya Kikosi Kazi;

vii) Kupunguza madaraka ya Msajili wa Vyama vya Siasa ili kuongeza uhuru wa vyama katika kujiendesha;

viii) Kuongeza uhuru wa kibajeti wa Tume ya Uchaguzi. Bajeti ya Tume itoke Mfuko Mkuu Hazina (Consolidated Fund) na sio kutoka katika Bajeti ya Serikali;

ix) Kuweka masharti kwa vyama ya kiwango maalum cha ushiriki wa wanawake kwenye vikao vya maamuzi; na

x) Kufanyika kwa mabadiliko madogo ya katiba (Minimum Reforms) ili kuiwekea miswada hii msingi madhubuti wa kisheria.

Aidha, Kamati Kuu imebainisha kuwa ni lazima mchakato wa Katiba Mpya uanze sasa. Serikali inapaswa kuweka wazi ratiba ya mchakato huo.

Kamati Kuu imeiagiza Kamati ya Uongozi Taifa kushirikiana na wadau wote wa demokrasia nchini kuweka shinikizo kuhakikisha miswada iliyowasilishwa inafanyiwa maboresho kuakisi maoni ya wadau ili kuimarisha uhuru wa kisiasa nchini na kuhakikisha chaguzi zinazokuja zinakuwa huru za haki na za kuaminika.

5. Mwenendo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar:

Kamati Kuu ya Chama Taifa ilipokea taarifa ya mwenendo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

Kamati Kuu imesikitishwa na mwenendo usioridhisha wa Serikali ya Kitaifa Zanzibar na kuelekeza hatua hadhaa madhubuti za kuchukua. Taarifa juu ya hatua hizo itawasilishwa wakati mwingine.

Mwisho, kwa niaba ya Chama cha ACT Wazalendo, ninapenda kutumia fursa hii kuwatakia Watanzania wote heri ya Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya.

Imetolewa na;

Ado Shaibu
Katibu Mkuu,
ACT Wazalendo,
21 Disemba, 2023.

Dar es Salaam.

Zitto Kabwe Anavyoitazama Tanzania ya 2050 Kiuchumi.Hapa anaandika Kiongozi wa ACT-WazalendoKatika mazungumzo yangu na M...
29/11/2023

Zitto Kabwe Anavyoitazama Tanzania ya 2050 Kiuchumi.

Hapa anaandika Kiongozi wa ACT-Wazalendo

Katika mazungumzo yangu na Maafisa Mipango na Wachumi wa Wizara, Idara, Mashirika ya Umma, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Nchi nzima wanaokutana hapa Arusha nimewaeleza kuwa Tanzania ya Mwaka 2050 itakuwa na Watu takribani milioni 130. Tukiweka lengo la kuwa na Pato la Mtu mmoja mmoja la USD 3,500 kwa Mwaka ifikapo 2050 ( zaidi ya mara mbili ya GDP/capita ya sasa ya USD 1200) tunahitaji Uchumi wa Tanzania uongezeke mara 6.5 hadi kufikia USD 455B.

Nimewaambia kuwa inawezekana kwani kati ya Mwaka 2000 na Mwaka 2022 GDP iliongezeka mara 5.8 kutoka USD 13B mpaka USD 75B.

Hivyo, kasi ya kukua kwa Uchumi inapaswa kuwa Wastani wa 8% kwa Mwaka kwa Miaka 10 ya mwanzo 2026-2036, na kasi hiyo isishuke 6% kwa Miaka mingine 15 mpaka Mwaka 2050.

Kasi hiyo ya ukuaji wa Uchumi itapaswa kuongozwa na sekta ya Kilimo, 6-8% kwa Mwaka. Nimesisitiza sana kuwa tunapaswa kuweka nguvu kubwa katika TIJA kwenye Kilimo ( angalau tuongeze mavuno mara mbili ( doubling ) ya sasa katika kila Ekari ya mazao ya Kilimo.

Nimewapa mfano wa zao la Pamba ambapo ilhali mkulima wa Tanzania anapata kilo 250-300 kwa kila ekari ya Pamba, mkulima wa Benin anapata kilo 800 na mkulima wa Burkinafaso anapata kilo 1500.

Hali ni mbaya zaidi kwenye Mahindi na Mpunga ambapo wakulima wetu wanapata gunia chache zaidi kutoka kila ekari 1!

Mambo ya kufanya wakati tunaandaa Dira mpya ya Maendeleo niliyopendekeza kwa wana mipango na wachumi;

1. Lazima tuwe na mjadala wa ukweli miongoni mwetu Watanzania bila ubaguzi wa kisiasa kuhusu Miaka 25 iliyopita. Je tulikuwa na mwafaka wa kitaifa kuhusu DIRA? Je tulikuwa na nidhamu ya kutosha kutekeleza DIRA 2025? Kwanini ilichukua Miaka 10 kuanza kutekeleza DIRA?
Tuwe tayari kukubali matobo na kuweka mikakati ya kuziba matobo hayo.

2. Baada ya tathmini ya hapo juu ( HONEST CONVERSATION), tujenge MWAFAKA WA KITAIFA kuhusu tunapotaka kuipeleka Tanzania. Lazima na ni muhimu kwa Watu wenye kufanya maamuzi na wenye ushawishi wa kimaamuzi ( viongozi wa Serikali, Watumishi wa Serikali, wanasiasa wa Upinzani, Wafanyabiashara, Watendaji wa Mashirika ya Umma, wakulima, wafugaji, Wavuvi, Wanafunzi etc) - Elite bargain, kukubaliana mwafaka wa kitaifa ( commitment to growth and development). Hii bargain
- ijenge makubaliano ya uhakika kuhusu Maendeleo
- kujenga dola lenye utayari wa kusaidia Maendeleo na sio predatory state
- ikubali kujifunza na kurekebisha makosa kila wakati yakitokea ( error correction).

3. Nimesisitiza kuhusu utekelezaji wa mipango ya Maendeleo kufikia DIRA.
- vipaumbele
- sequencing ( nini kinaanza na nini kinafuata)
- nidhamu ya utekelezaji

Nimewakumbusha kuwa Jiografua yetu pekee inaweza kuifanya Nchi yetu kuwa na mapato ya kigeni ya zaidi ya USD 12B kwa Mwaka na makusanyo ya kodi ya USD 10B kila Mwaka kutoka katika Forodha peke yake. Hivyo ufanisi wa Bandari utumike kusaidia sekta nyengine.

4. Nimewakumbusha kuwa Tanzania inahitaji kujenga uwezo wa ndani wa mitaji ili sekta Binafsi ipate mitaji ya kuwekeza katika kukuza Uchumi. Uwezo wetu wa ndani wa kuweka akiba ni mdogo. Savings - GDP ratio ni chini ya 16%. Hivyo nimeshauri kujenga mfumo madhubuti wa Hifadhi ya Jamii ( social security) ili kujenga uwezo wa Watu wetu kuweka Akiba.

Nimewakumbusha kuwa Watanzania wengi ni masikini na wengi wao wanazunguka Mstari wa umasikini. Walio juu wakipata shock kidogo wanadondoka, waliochini wakipata boost kidogo wanapanda. Wajibu wa Uongozi ni kuwapandisha waliochini na kuwahami waliojuu wasidondoke. Hifadhi ya Jamii kwa wote ndio jawabu ya hilo.

NIMESISITIZA
- pale ambapo sekta Binafsi inafanya vizuri, Serikali isiingilie. Serikali iweke sera nzuri na kutekeleza Sheria.
- uwiano kati ya Uchumi na siasa uzingatiwe. Tukishajenga mwafaka wa Maendeleo Basi Vyama vya siasa Bisho sane kuhusu mikakati ya utekelezaji ili kufikia DIRA.

Address

Kigoma Manispaa
Kafr Al-Dawar

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kigoma Yetu DamDam posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Kigoma Yetu DamDam:

Share

Category