31/12/2023
MWENYEKITI UVCCM ASIKITISHWA NA VIONGOZI WASIOHUDHULIA VIKAO VYA CHAMA.
Mwenyekiti Wa Jumuia Ya Vijana (UVCCM) Wilaya Ya Bagamoyo, CDE. Hafidhi Nassoro Konyamale amesikitishwa na Baadhi ya Viongozi Wasiofika Katika Vikao Vya Mabaraza ya Chama Cha Mapinduzi .
Hayo Ameyasema Jana Wakati Akiongea Na Wajumbe Wa Baraza La Uvccm Wilaya ya Bagamoyo Wakati akiwa Katika Baraza La Uvccm Wilaya Ya Bagamoyo Lililofanyika Katika Viwanja Vya Shule ya Sekondari Kibindu, Kata Ya Kibindu Halmashauri ya Wilaya Chalinze.
"Binafsi Sijaridhishwa na Wajumbe Wa Baraza Ambao Hawakufika Katika Baraza Hili, Kwani Moja Ya Nguzo Imara Ya Chama na Viongozi Wake Ni Kushiriki Vikao Vya Jumuia Pamoja na Mabaraza Yake. Baraza Hili Lipo Kikanuni Ndani Ya Jumuia Yetu, Lengo Ni Kuangalia Mafanikio Ya Jumuia Katika Muhura Wa Pili Wa Mwaka Na Wapi Paboreshwe Ili Kuongeza Ufanisi Katika Jumuia Yetu ya Vijana Wilaya Ya Bagamoyo " Amesema
Mwenyekiti Huyo Ameongeza "Fikilia Kiongozi Hafiki Kwenye Kikao Cha Baraza, Je Tutajuaje Changamoto Anayokutana Nayo Tunapohitaji Taarfa Za Utekelezaji Ndani Ya Eneo Lake?? Kiufupi ni Kitu Kisichoridhisha Kwani Viongozi K**a Hawa Ndio Wataokwamisha Ilani Ya Chama Katika Kutekeleza Ilani Yake "
Pia Mwenyekiti Huyo Ameelezea Mikakati Ya Jumuia Hiyo kuelekea Uchaguzi Mdogo Wa Diwani Katika Kata Ya Fukayosi Utaofanyika Mwezi February Kufuatia Kifo Cha Aliyekua Diwani Wa Kata Hiyo Ally Ally Aliyefariki Dunia Siku Za Karibuni. Hivyo K**a Wanajumuia, Wanatakiwa Kuhakikisha Kua Chama Chao Kinarudi Katika Kiti Cha Kuiongoza Kata Hiyo.
CDE Konyamale Amezitaja Baadhi Ya Kata Zilizoonesha Uhafifu Wa Ushiriki Katika Baraza Hilo Kua Ni Kata Ya Kiwangwa, Ubena, Vigwaza, Fukayosi Huku Kata Ya Msata Ikiwakilishwa na Mwenyekiti, Katibu Pamoja Na Katibu Hamasa Pekee. Wakati Huo Huo Kata Ya Talawanda Pamoja na Pera Zikiwa Na Idadi Nzuri Ya Viongozi Walioshiriki Baraza Hilo .
Jana Jumuia Ya Vijana Wilaya ya Bagamoyo Imefanya Kikao Cha Pili Cha Baraza Kwa Mwaka 2023 Ambalo Lipo Kikanuni Katika Kata Ya Kibindu Halmashauri ya Wilaya Chalinze Ambapo Kabla Ya Kufanyika Kwa Baraza Hilo,Aliweza Kutembelea Kituo Cha Afya Kibindu Pamoja Na Kupanda Miti, Kutembelea Soko La Kibindu Na Baadae Kufanya Mkutano Wa Hadhara Na Wanakijiji wa Kata Ya Kibindu.
Uvccm Magomeni Bagamoyo
UVCCM Bagamoyo
Uvccm Mapinga
Uvccm Kata Ya Talawanda
Uvccm Kata Ya Msata
Uvccm Kata Ya Kiwangwa