14/03/2024
MPANGAJI ANAHESABIKA NI MVAMIZI MARA TU KODI YAKE INAPOISHA.
Tarehe 5/10/2022 majaji watatu wa Mahak**a ya Rufaa kupitia Rufaa Na. 333/2019 kati ya Lawrence Magesa t/a Jopen pharmacy VS Fatuma Omary na Rimina Auction Mart wamesema kuwa pale mpangaji kodi yake inapoisha na akawa hajaondoka katika nyumba ama eneo la pango, basi hadhi yake inabadilika na anakuwa mvamizi(trespasser).
Kwa sheria zetu mvamizi anaweza kuondolewa ndani nyumba/eneo kwa nguvu yeye na mali zake bila hata kuhitaji notisi.
Na akiondolewa kwa nguvu yeye na mali zake hawezi kudai fidia ikiwemo ile ya kwamba nilikuwa na milioni 10 zangu ndani wakati naondolewa zimepotea.
Hukumu hii inasema hawezi kudai kwasababu kuendelea kwake kuwemo ndani wakati kodi yake imeisha ni makosa na hivyo hawezi kuwa mnufaika wa makosa yake mwenyewe(benefit from own wrongs).
Na huu ndio msimamo wa sheria hata kabla ya hukumu hii. Wapangaji wajifunze kuwa wapole kodi zao zinapokuwa zimeisha. Kodi inapoisha unapoteza haki za upangaji.
Kuhusu notisi ya kuondoka, mpangaji ambaye kodi yake imeisha hapewi notisi isipokuwa k**a mkataba wake unasema hivyo.
K**a hausemi hivyo basi kodi ikiisha ni kuondoka, ama kuondolewa kwa nguvu, ama kuomba vinginevyo kutoka kwa mwenye nyumba/eneo.
Mahak**a ya rufaa ndiyo mahak**a kubwa na ya juu kuliko zote Tanzania, na ndiyo inaongea maneno haya.
Mwisho nasisitiza, ile habari ya kuondolewa kwa nguvu ukitegemea utasema milioni 10 yangu iliyokuwa kabatini nayo imepotea sahau. Ni maneno ya mitaani hayo achana nayo yatakupotezea muda.
Huwezi lipwa, kwani tangu kodi yako ilipoisha ulikuwa mvamizi na mvamizi halipwi manufaa na stahiki k**a hizo.
Follow pages zetu Facebook, Instagram, Twitter, LinkedIn, YouTube
Read writing from Hamia Hapa on Medium. Washauri wa Ramani & Ujenzi wa Nyumba & Miradi 0768630333. Real Estate Development & Management, Land & Environment Advisory 0744112003.