13/10/2026
Ardhi sio UTT! Na zingatia ardhi ya jumla inalipiwa kodi ya ardhi...π
Swali ni je, unaijua ardhi ya jumla?
K**a huijui, vuta kiti upate madini...βοΈ
Kwa mujibu wa sheria za ardhi nchini Tanzania, ardhi imegawanywa katika makundi makuu matatu:
Ardhi ya Kijiji
Ardhi ya Hifadhi
Ardhi ya Jumla
Sasa leo naomba twende na ARDHI YA JUMLA.
Ardhi ya jumla ni ardhi ambayo haijaainishwa k**a ardhi ya kijiji au ardhi ya hifadhi, Ardhi hii inapatikana maeneo mbalimbali yakiwemo maeneo ya mijini na pembezoni mwa miji.
Ardhi hii inasimamiwa kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi sura 113, na moja ya mambo muhimu unayopaswa kufahamu ni suala la kodi ya ardhi.
Kwa kawaida, mwenye haki ya kumiliki ardhi kupitia hati miliki yenye masharti ya kulipa kodi ya ardhi anatakiwa kulipa kodi hiyo kwa mujibu wa masharti yanavyomtaka.
Hii ina maana kwamba unapowekeza kwenye ardhi, si suala la kununua kiwanja tu. Ni muhimu pia kufahamu wajibu unaoambatana na umiliki wako, ikiwemo kodi ya ardhi inapohusika...
Kumbuka, kuwekeza kwenye ardhi ni zaidi ya kumiliki kiwanja; ni kuelewa haki zako na wajibu wako k**a mmiliki.
swali, Je, unajua masharti ya umiliki wa ardhi yako?
Comment & Share na mwingine ajue.
TUPO KUTIMIZA MALENGO YAKO!
β 0718 395 914
πPrime location
π100% free title deed.
πππππππ ππππ ππππππππππ ππ πππ πππππππ ππππ ππππππππππ ππ πππ