Jadi Tunataka watu waishi kiimani zaid

27/03/2022

Ccoment ili kila m2 ajue kua nmcomnt illa nacomnt il kila aonae amaanish nikicho coment ®HVYO BC UCKUBL HATA CKU 1 MWANA SIASA ANAPO KWAMBIA UCK MWMA TOKA NJE KWANZA UONE NIKWER KIZA KIMEINGIA©

20/06/2021

DUA BAADA YA KULA
Alhamdu lillahilladhii atwa amanii hadhaltwa aam walazakanihi!

20/06/2021
20/06/2021

KARIBUNI KWAJILI YA DUAT AINA ZOT

Tunataka watu waishi kiimani zaid

20/06/2021

DUA YA KULA
Bismillahi

15/03/2021

WAFAHAMU MALAIKA NA KAZI ZAO..

JIBRIIL

Huku ni Malaika mkubwa kabisaa kati ya Malaika wote aliyowaumba ALLAH (Subhaanahu wa Ta'ala) Malaika huyu ana mbawa takribani 600. Kazi kubwa ya Malaika huyu ni kuteremsha Wahyi (ufunuo) kwa Mitume, tokea kwa Adamu (Alayhis Salaam) mpaka Mtume wa mwisho Muhammad (Swalla ALLAHU alayhi wa sallam)
MALAKUL MAUTI

Huyu ni Malaika maarufu sana kufahamika kwa watu wengi. Malaika huyu amepewa jukumu na ALLAH (Subhaanahu wa Ta'ala) la kutoa Roho (Nafsi) za watu. Malaika huyu kapewa uwezo wa kuingia popote pale ili kutoa Roho ya mtu ambaye muda wake umeshafika wa kuondoka hapa duniani, hata k**a mtu huyo awe na ulinzi kiasi gani. ALLAH amemtaja Malaika huyu kwenye Qur'an pale aliposema, "Sema: Atakufisheni Malaika wa Mauti aliyewakilishwa kwenu, kisha mtarejeshwa kwa mola wenu." Surat Assajida: 11.

RAQIIB NA A'TIID

Hawa ni Malaika wawili mmoja anakaa upande wa kulia wa mwanadamu na mwengine anakaa upande wa kushoto wa mwanadamu. Kazi yao kubwa ni kuandika matendo (Amali) ya wanaadamu. Wa kulia anaandika matendo mema na wa kushoto anaandika matendo maovu. Popote utakapokwenda hawa Malaika unao, utakachosema au utakachofanya kiwe kibaya au kizuri hawa Malaika wanakiandika. ALLAH(Subhaanahu wa Ta'ala) amewataja Malaika hawa kwenye Qur'an pale aliposema, " Hatoi kauli yoyote (mwanaadamu) isipokuwa karibu naye yuko mngojeaji tayari (kuandika)." Qur'an (50:18).

👉MUNKAR NA NAKIIR

Hawa nao pia ni Malaika wawili wanaopatikana katika maisha ya barzakh (Maisha ya kaburini). Na kazi yao kubwa ni kuwauliza watu maswali ndani ya kaburi baada tu ya kuzikwa kwao (mtu). K**a ulikuwa mwema hawatokudhuru, lakini k**a ulikuwa muovu watakudhuru tu.

👉ISRAAFII
Huyu ni Malaika ambaye kazi yake kubwa ni kupuliza baragumu (parapanda) siku ya Qiyama. Inasemekana tokea aumbwe Malaika huyu hakuwahi kutoa pumzi nje, ila kazi yake ni kuingiza pumzi ndani. Atakuja kuitoa siku ya kiama pale atakapoamrishwa apulize baragumu siku ya Kiama.

👉MAALIK

Huyu ni Malaika wa motoni na kazi yake kubwa ni kuwaadabisha madhalimu na watenda maasi,maovu na machafu. Huyu malaika tangu aumbwe hajawahi kucheka wala kutabasamu, ila alikuja kutabasamu baada ya Mtume kufika mbinguni, na Mtume mwenyewe hakujua k**a kaoneshewa tabasamu ambapo alimuuliza Jibriil (Alayhis Salaam) mbona Malaika wote wanaonesha furaha juu yangu lakini mmoja tu haoneshi furaha, Jibriil akamwambia tena hapo katabasamu baada ya kukuona wewe kipenzi cha ALLAH (Subhaanahu wa Ta'ala) Sasa jiulize mimi na wewe?. Tufanye toba kwa wingi na tumtii ALLAH na Mtume wake.

RIDHWAAN

Huyu ni Malaika wa peponi, na kazi yake kubwa ni kuwakaribisha waja wema kuingia peponi na kuwariwadha kutokana na mitihani waliyokutana nayo duniani.

MIKAAIL

Huyu ni Malaika mwengine ambaye kazi yake kubwa ni kuteremsha Mvua. Kila tone moja basi linawakilishwa duniani na Malaika mmoja wakiongozwa na Mikaail.

WABILLAHI TAWFIIQ.
K**A KUNA SEHEMU NIMETEREZA MIMI NAYE NI BINADAMU, HAKUNA MKAMILIFU BALI UKAMILIFU NI WA ALLAH (Subhaanahu wa Ta'ala).

Uislamu Dini Yangu

07/03/2021

Karbu jad

07/03/2021

KARBU JAD

Address

Kwazena
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jadi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category