31/07/2021
🛑 *UJUE UGONJWA WA P.I.D*
Maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa kitaalamu Pelvic Inflamatory Diseases au kwa kifupi PID, ni moja ya matatizo ambayo huwaathiri sana wanawake. Kwa kawaida maambukizi haya huusisha shingo ya uzazi (cervix) hali ambayo hujulikana k**a cervicitis, nyama ya mfuko wa uzazi (endometrium) ambayo kitaalamu huitwa endometritis, na mirija ya uzazi (fallopian tubes) hali ijulikanayo kitabibu k**a salpingitis.
*_PID husababishwa na nini?_*
Pamoja na aina kadhaa za vimelea kuhusishwa na PID, vimelea vya jamii ya Neisseria Gonorrhoeae pamoja na Chlamydia trachomatis ndivyo vinavyoongoza kwa umaarufu zaidi katika kusababisha PID kwa akina mama.
*Je mwanamke huambukizwaje PID?*
Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa PID. Njia hizo ni pamoja na
✅Kufanya ngono isiyo salama.
✅Maambukizi ya njia ya uzazi hasa kipindi mara baada ya kujifungua (au postpartum period)
✅Maambukizi ya njia ya uzazi mara baada ya kutoa mimba kwa njia zisizo salama (post abortion) au mara baada ya mimba kutoka (miscarriage)
✅Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi (IUCD) k**a njia mojawapo ya uzazi wa mpango.
✅Kuambukizwa kupitia damu iliyo na vimelea vya PID.
*Dalili za PID ni zipi?*
Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID. Miongoni mwa dalili hizi ni :-
✅Mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu
✅Kupata maumivu ya mgongo.
✅Mwanamke kupata utoko mchafu sehemu za siri. Utoko huu huambatana na harufu mbaya.
✅Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa.
✅Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.
✅Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi.
✅Kupata homa.
✅Wakati fulani kuhisi kichefuchefu na
Pia kutapika.
⏩Ugonjwa huu wa Pelvic Inflammatory Diseases *P.I.D* unakuwa kwa Kasi kubwa na baadhi ya wanawake hupata madhara makubwa baadae hususani Ugumba kutokana na kupuuzia matibabu. Ikiwa unaona dalili tajwa hapo juu jitahidi kuanza matibabu taratibu kabla haujapata madhara ambayo yanaweza kugharimu Maisha yako kwa ujumla.
✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿
*MUWE NA MCHANA ULIO MWEMA NYOTE, JIKINGE NA P.I.D epuka UGUMBA*