23/07/2026
Ni heshima kubwa kwa Property International Ltd kupata fursa ya kumkabidhi Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, taarifa ya tuzo tatu tulizotunukiwa katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Saba Saba) 2026.
Katika mazungumzo hayo, tulipata pia maelekezo na ushauri wenye thamani kuhusu kuendelea kuimarisha sekta ya uwekezaji wa ardhi na makazi kwa kuzingatia ubora, uadilifu na maendeleo endelevu.
Property International inaendelea kujikita katika kuendeleza miradi inayolinda na kuhifadhi mazingira kupitia upangaji bora wa matumizi ya ardhi, utunzaji wa maeneo ya kijani, upandaji wa miti, na kuhakikisha maendeleo tunayoyaleta yanakwenda sambamba na uhifadhi wa mazingira kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa muda wake, maelekezo yake na kututia moyo kuendelea kujenga Tanzania yenye maendeleo jumuishi na endelevu.
RealEstate InvestInTanzania