15/09/2026
Hela sio kitu cha kukiwazia kila saa na kuruhusu kikunyime raha ama amani.
Unakuta mtu maisha yake yote ana mashaka na wasiwasi kuhusu pesa japo ana ndoto na hamu ya kuwa tajiri.
Hautafanikiwa k**a utaruhusu KUWA MTU WA MASHAKA NA WASIWASI KISA PESA.
Ukiruhusu kua na wasiwasi kuhusu pesa na mashaka kuhusu pesa maana yake umeiambia pesa ikutawale
Umeiambia pesa kua wewe ni mtumwa wake.
Na pesa ikikutawala, utaanza kuogopa kila kitu. Utaogopa kutumia, utaogopa kusaidia wengine, utaogopa kuwekeza, na mwisho unaweza ukakosa kufanya mambo mengi muhimu kwa sababu tu unaogopa kupungukiwa.
Wewe ndiye unapaswa kuitawala pesa, sio pesa ikutawale wewe.
Tumia pesa bila hofu ya kupoteza, lakini kwa akili na mipango.
Utaona pesa zitakavyokuwa zinajileta kwenye maisha yako.
Saidia wengine bila hofu kwamba utakuja kufilisika.
Utaona milango ya baraka inavyomiminika kwako.
Wekeza bila kuogopa kwamba kesho hutakuwa na kitu ama utapoteza uone namna fursa zitakavyokuwa zinajileta kwako na katika muda sahihi.
Fanya biashara bila kuishi na hofu ya kila hela inayotoka ama kuwaza utapata hasara uone namna biashara hiyo itakavyofanikiwa.
Unachopaswa kutambua ni kuwa pesa ni chombo cha kukusaidia kufika unapotaka kwenda. Sio kitu cha kukufanya uishi maisha ya hofu.
Lakini kuitawala pesa haimaanishi kuitumia hovyo.
Ni kujua hela yako inatoka wapi, inaenda wapi na kwa nini.
Ukipata nyingi, usione imetosha
Ukipata kidogo, usione umekosa na kuanza kupata stress.
Ukipoteza, usikate tamaa.
Ukipata faida, usitumie yote.
Jifunze kuweka akiba.
Jifunze kuwekeza.
Jifunze kutumia.
Jifunze kusaidia.
Na zaidi ya yote, jifunze kutengeneza tena pesa inapopotea.
Usiishi maisha ya kuogopa kuishiwa pesa kwasababu hautakua na furaha na hiyo pesa hata ukiipata.
Na wakati mwingine, tatizo sio kwamba huna pesa. Tatizo ni kwamba akili yako imezoea kuishi kwenye hofu ya kuishiwa.
Hautafurahia unachopata kwa sababu kila siku unaogopa na kuwaza kuhusu kesho huamini kuwa kesho yako ni njema na mafanikio ni haki yako.
Na kwa kuwa kila hela unayoipata unaiona k**a ndio ya mwisho, utaishi maisha ya kujilinda badala ya maisha ya kujenga.
(Ukitaka kutambua hasara za kujilinda fatilia mchezo wa mpira wa miguu uone wachezaji wanavyoamua kupaki basi mara nyingi huishia kufungwa)
Pia Kuna wakati pesa itabidi itoke ili ikuletee pesa nyingine.
Kuna wakati utapaswa kutumia pesa kujifunza huku ni kulipa gharama na kukua si umesikia kuwa mafanikio ni gharama?
Miongoni mwa gharama ni pamoja na kujifunza.
Kuna wakati utatumia pesa kusaidia mtu hii pia ni moja ya kazi ya pesa.
Na kuna wakati utapoteza pesa ni kitu cha kawaida kabisa kwenye mafanikio.
Kwenye kupoteza kuna kujifunza, na kwenye kujifunza kuna kupata.
Jambo la msingi ni kuhakikisha pesa inapita mikononi mwako, sio kukaa moyoni mwako.
Sio usiku usilale kisa unawaza hela.
Ukiamka huwazi kingine zaidi ya hela.
Ukipata hela unaogopa kuitumia eti itaisha.
Kwasababu ulipoteza hela ama uliibiwa basi usianze kila mtu kumuona ni mwizi,
Na kwasababu ulitapeliwa usianze kuona kila fursa unayoambiwa ni ya utapeli.
HAIKO HIVYO!
HAIKO HIVYO!
Anza kupona.
Tengeneza uhusiano mzuri na pesa.
Itafute kwa bidii.
Itunze kwa nidhamu.
Itumie kwa hekima.
Iwekeze kwa akili.
Igawanye kwa moyo.
Na iache ikufanyie kazi.
Usikubali kuwa mtumwa wa pesa.
Kwa sababu ukiwa mtumwa wa pesa, utaishi maisha ya hofu badala ya maisha ya kujenga.
Kuanzia leo, ifanye pesa iwe mtumishi wako.
Itumikishe ikuletee pesa nyingine.
Itumikishe ikujengee mali.
Itumikishe ikufungulie fursa.
Itumikishe ikusaidie watu.
Itumikishe ikupe uhuru.
Lakini wewe ndiye ubaki kuwa bosi.
PESA IKUTUMIKIE WEWE na WEWE USIITUMIKIE PESA.
Na kila unapopata pesa, usijiulize tu, โNitaipata wapi nyingine?โ
Jiulize pia:
โNitaifanyisha nini hii pesa ili iniletee pesa nyingine?โ
Hapo ndipo unaanza kubadilisha uhusiano wako na pesa.
Hapo ndipo pesa inaanza kuwa chombo cha kujenga maisha unayoyaota.
Nakuombea uponyaji ushinde hofu na ufanikiwe kwenye kila kitu ๐ฅฐ๐
KARIBU SANA gulio la ardhi
Miliki Mashamba chalinze Ekari kuanzia 750,000,Bandari kavu vigwaza ekari kuanzia Milioni 6,Bagamoyo Ekari kuanzia milioni 1 na nusu,gumba gwata laki 5 na 80 ๐๐๐๐๐ฅ๐ฅ๐ฅ
0746465095
0675719930