17/08/2023
UNAWEZA KULOGWA HATA K**A UMEOKOKA
Huyu Baba Yangu Mzazi Archbishop Enos A. Nkone, tangu nikiwa mtoto mdogo Nilikuwa Naona kwa macho yangu Akiwatoa pepo Washirika weeengi na Wachungaji waliokuwa wanalogwa. Kaka yangu Bishop David Nkone anafanya huduma hii kwa miaka mingi sana sasa. Mimi mwenye nikishirikiana na mke wangu Pastor Nnunu ni miongoni mwa Watumishi Weengi sana ambao Tumeendelea mpaka sasa na huduma hio ya Kutoa pepo au Kuvunja vitungo vilivyowekwa na walozi/wachawi kwenye maisha ya watu mbalimbali wakiwemo wakristo waliookoka.
Wapo Wengine ambao Kinachologwa sio Afya zao, ni Ndoa zao, au Biashara zao, au Watoto wao, au Mashamba yao, au Kazini, Mwingine analogwa asizae au asipate mimba, mwingine analogwa asiolewe/asioe, mwingine analogwa Akili asisome, asimalize Masomo, Mwingine Uchumi wake Unalogwa asifanikiwe katika kila Biashara anayofanya, Uwanja wa Mkutano wa Injili unaweza Kulogwa mpaka ukakuta mambo mbalimbali hapo kwenye Mkutano yanavurugika, umeme unakatika bila sababu, mvua inaweza kunyesha, upepo mkali unaweza kuvuma kuvuruga Mkutano, n.k
Kupagawa na mapepo sio dalili peke yake kwamba mtu amelogwaa. Kuna Kulogwa kwa aina Kuu Mbili:
(1) Afya yako (2) Mambo yote Yanayokuhusu,
AFYA YAKO.
Sio lazima upagawe na mapepo. Unaweza ukapigwa ulozi ukapatwa na vidonda au majipu, au kupungukiwa na damu, au Kupata ajali za ajabu-ajabu, au Kuchukiwa/Kukataliwa, n.k.
MAMBO YOTE YANAYOKUHUSU
Biashara yako inaweza Kulogwa au Vitega Uchumi vyako, Ndoa yako inaweza Kulogwa, Shamba linaweza Kulogwa, Ujenzi wa nyumba yako, Gari lako au Lori lako au Trekta lako linaweza Kulogwa. Nyumba unayoishi inaweza kulogwa,
Ninaandika haya from Experience, not just Theology. Watumishi woote Wenye huduma ya Deliverance Huwa Wanacheka Wakimsikia Mtumishi anasema kwamba WALIO-OKOKA HAWAWEZI KULOGWA. Pia hata Wapendwa Waliookoka na waliwahi Kulogwa wakiwa Wameokoka, au hata sasa bado wamelogwa na Wameokoka, wakimsikia Mtumishi anasema kwamba WALIO-OKOKA HAWAWEZI KULOGWA Wanacheka na Kumshangaa saaana Mtumishi anaesema hivo.
KWA NINI ALIEOKOKA ANAWEZA KULOGWA?
Shetani, Mapepo au Mlozi/Mchawi, huwa anatafuta “LEGAL ACCESS (UHALALI)” ili aweze kuloga. Mlozi/Mchawi anaweza kukuloga akipata Uhalali au mlango. Pia Shetani mwenyewe anaweza kukuloga kwa Kuyatuma mapepo ya Rank/ngazi mbalimbali yakusumbue au kuzuia baraka zako, huduma yako, maombi yako (Daniel 10:13), kukutesa (Luka 22:31, Job/Ayubu 1:1 - 2:13). Pia Shetani anaweza kumuua Mtumishi wa MUNGU (Ufunuo 2:13 “Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.” Matthew/Matayo 14:6-12 Yohana Mbatizaji alikatwa Kichwa na Shetani kwa kumtumia Mfalme Herode.
Ephesians 4:27-29 Mtume Paulo anawaambia Waefeso waliookoka kwamba Wasimpe shetani nafasi. Shetani yeye mwenyewe, au kwa Kupitia Ma-Agent wake Ukimpa nafasi unakuwa umempa UHALALI (LEGAL ACCESS) ya kukushughulikia. Dhambi ni mlango mkuu, na dhambi zipo za aina nyingi including dhambi ya Kutokuaminu, Hasira, wivu wa Siri na Kutofurahia mafanikio ya mwingine, uchoyo, ubinafsi, au mpendwa hatoi sadaka makusudi, n.k
Mimi Donis Nkone nilishawahi Kulogwa mara nyingi. Kijana wangu Salvation Leonard akiwa ameokoka Walimloga vibaya saana. Na hata sasa bado Walozi wanamsumbua sana.
Galatians 3:1-14 Mtume Paulo aliwauliza Wapendwa Wagalatia waliookoka “Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?” Hawa Wagalatia Walilogwa na baada ya Kulogwa Walianza Kufanya Mambo ya ajabu-ajabu yaliyomfanya Paulo aone k**a Akili zao zimelogwa.
Job 1:1 - 2:13 you will see how Satan afflicted Job who was a Perfect Man according to the scriptures. Ayubu aliteswa saana na Shetani hata k**a Biblia inasema “alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.” Hapa ni MUNGU alimruhusu/alimpa shetani Legal Access/Uhalali.
Matthew/Mathayo 8:23-27 anasema “Kukawa msukosuko mkuu baharini, hata chombo kikafunikizwa na mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi. 25 Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana, tuokoe, tunaangamia.” Lazima Uelewe kwamba Ndani ya ule msukosuko mkuu baharini kulikuwa na pepo waliokuwa wanamzuia Yesu na Wanafunzi wake. Wapo wapendwa weengi saana Wanapitia msukosuko mkuu maishani, kazini, kwenye ndoa, n.k. kwa sababu Wamelogwa wasiende mbele au wasifanikiwe.
Hawa Watumishi wote; Askofu Moses Kulola, Archbishop Duncan Williams, Mwalimu Mwakasege, wote wame experience Kulogwa (sio kupagawa na pepo) na pia Wamewaombea Wapendwa weengi waliokuwa Wamelogwa.
Ingawa Dhambi ni mlango (legal access) ya kwanza, lakini pia sio dhambi peke yake ndio mlango. Hata kuwa na mtu maarufu sana, au mzuri saana, au Mwombaji sana, au Mkamilifu sana mbele za MUNGU, au mwenye nyota kubwa, au Mchungaji mwenye nguvu ya MUNGU, vyooote hivi vinaweza kuwa Mlango. Ndio maana unaweza kukuta Mtoto mdogo saana amelogwa.
(Nitarudi Kuendelea . . . )