28/05/2023
Tuzungumze "Faida za Uwekezaji kwenye Mali isiyohamishika" au Real Estate kwa Kiingereza.
Uwekezaji kwenye "Mali isiyohamishika" k**a ilivyo kwenye aina nyinginezo za uwekezaji, huja na changamoto nyingi ikiwamo kushuka thamani ikiwa makadirio na hesabu hazikufuatwa sawasawa. Hilo tutakuchanganulia ukitutumia sms, WhatsApp ama DM kwa maswali.
REITs (Real Estate Investment Trusts), ni amana za uwekezaji wa mali isiyohamishika, na ni mojawapo ya njia rahisi zaidi za kuwekeza katika mali isiyohamishika. Kwa nini? Ukiwa na REIT, unawekeza katika mali isiyohamishika bila kuwa na wasiwasi kuhusu kutunza, kuendesha au kusimamia majengo husika, kazi hiyo hufanywa na kampuni zinazomiliki mali isiyohamishika, kitu chochote kuanzia fremu za Biashara ya rejareja hadi majengo ya ghorofa, hoteli, ofisi au maghala.
Unaponunua katika REIT, unanunua sehemu ya mali hizi. Ni kidogo k**a kuwekeza kwenye hazina za kawaida (mutual funds), au Biashara ya hisa, isipokuwa REIT inahusika na mali isiyohamishika. Unaweza kupata pesa kutoka REIT kwa njia mbili: Kwanza, REIT hufanya malipo ya gawio ya kawaida kwa wawekezaji. Pili, ikiwa thamani ya jengo ama mradi husika itaongezeka, unaweza kuuza uwekezaji wako kwa faida. Unaweza kuwekeza kwenye REIT k**a kuwekeza kwenye hisa: REIT huweza hata kuorodheshwa kwenye soko kuu la hisa kupitia "Uwekezaji wa Majengo", biashara ambayo haijawa kubwa hapa Tanzania.
Faida zake huonekana kupitia malipo ya kila mwezi kupitia makusanyo ya Kodi, gawio kutokana na faida za jumla, na pia uhakika wa faida ikiwa thamani ya jengo hupanda na kuuzwa kwa faida zaidi ya makadirio.
Kwa maswali, maoni na ushauri. Tutumie sms, WhatsApp au DM kwenye mitandao ya kijamii.
TanMark, njoo tuzungumze