Agriworth Tanzania Company ltd

Agriworth Tanzania Company ltd Agriworth Tanzania Company Ltd ,Deals with Export of Agricultural products and farm management services in Tànzania. Addresses;
P.O.BOX 163,
Njombe,Tànzania.

Call/WhatsApp+255766766718
Email, [email protected]

USISUBIRI UGONJWA UENE NDANI YA BANDA LAKO! Hasara kubwa kwenye ufugaji wa kuku si gharama ya chakula pekee, bali ni mli...
05/07/2026

USISUBIRI UGONJWA UENE NDANI YA BANDA LAKO!

Hasara kubwa kwenye ufugaji wa kuku si gharama ya chakula pekee, bali ni mlipuko wa magonjwa. Kuku mmoja mgonjwa anaweza kuambukiza wengine kwa muda mfupi na kukusababishia hasara kubwa.

Dalili 4 za Awali za Kuku Anayeanza Kuugua

🔴 1. Mabadiliko ya Utosi (Comb) Utosi wa kuku mwenye afya huwa mwekundu na wenye nguvu. Ukianza kufifia, kupauka au kunyauka, hiyo ni ishara ya tatizo la kiafya.

🥣 2. Mabadiliko ya Tabia Kuku mwenye afya hula, hunywa na kuchangamana na wengine. Kuku mgonjwa hujitenga, hukosa hamu ya kula na huwa mnyonge.

🪽 3. Mabadiliko ya Mwonekano Angalia k**a mabawa yamelegea, mkia umeshuka, macho yamelegea au eneo la haja kubwa limechafuka. Hizi ni dalili zinazohitaji uchunguzi wa haraka.

💩 4. Mabadiliko ya Kinyesi Kinyesi cha kawaida huwa kigumu na chenye sehemu nyeupe juu. Kinyesi cha maji, kijani, njano au chenye damu ni ishara ya ugonjwa na kinahitaji hatua za haraka.

Ukiona Dalili Hizi, Fanya Haya Mara Moja:

✅ Mtenganishe kuku mgonjwa na wengine. ✅ Mpe maji safi na vitamini ili kupunguza msongo. ✅ Safisha na ua vijidudu kwenye banda, vyombo vya chakula na maji. ✅ Wasiliana na mtaalamu wa mifugo kwa uchunguzi na matibabu sahihi. Epuka kutumia dawa kwa kubahatisha.

Kuzuia ni nafuu kuliko kutibu. Dumisha usafi wa banda, punguza msongamano, dhibiti wageni wanaoingia shambani na fuata ratiba ya chanjo.

MBEGU BORA YA NYANYA SVTE8444F1●Ina uzaaji mwingi hata kwenye maeneo yenye magonjwa k**a viruses, kutu, bakajani, ubwiri...
05/07/2026

MBEGU BORA YA NYANYA SVTE8444F1

●Ina uzaaji mwingi hata kwenye maeneo yenye magonjwa k**a viruses, kutu, bakajani, ubwiri unga. Ina uwezo mkubwa wa kuvumilia magonjwa haya na kuleta matokeo mazuri.

●Inavumilia magonjwa sugu ya viruses ambayo hupunguza sana uzalishaji kwenye nyanya k**a-
Tomato spotted wilt viruses (TSWV)
-Tomato yellow leaves curly viruses (TYLCV)
-Tomato mosaic viruses (ToMV)
-Tomato Torrado viruses (ToTV)

●Ina matunda makubwa, gm (150-160) michumo mingi (hadi miezi 4) na matunda yake hayapungui ukubwa mwanzo hadi mwisho wa mchumo.
● Inapunguza matumizi makubwa ya viuatilifu kwa kuwa ina ukinzani mkubwa wa magonjwa yanayosambazwa na thrips na vipepeo na minyoo fundo (nematodes). Reduce production cost.
● Inafaa kiangazi na kwenye mvua pia kwa kuwa na uvumilivu mkubwa wa magonjwa ya kuvu.

Mfugaji anaposema, “kuku wangu mmoja amezubaa na hana uchangamfu,” hiyo ni hatua nzuri ya uangalizi, lakini ni mwanzo tu...
04/07/2026

Mfugaji anaposema, “kuku wangu mmoja amezubaa na hana uchangamfu,” hiyo ni hatua nzuri ya uangalizi, lakini ni mwanzo tu — haitoshi kwa uchunguzi sahihi wa tatizo.

Kwa ufugaji wa kuku, maelezo ni chombo cha kwanza cha tiba.
Maelezo duni husababisha utambuzi usio sahihi, na utambuzi mbaya hupelekea dawa zisizo sahihi, upotevu wa fedha, na wakati mwingine vifo vya kuku.

Badala ya kuishia kusema “kuku amezubaa,” mfugaji makini anatakiwa aeleze mambo k**a haya:

✅ Umri wa kuku
✅ Anakula na kunywa k**a kawaida au amepunguza?
✅ Kinyesi kikoje (cha kawaida, kijani, maji maji, chenye damu, cheupe?)
✅ Upumuaji (anakohoa, anapiga chafya, anapumua mdomo wazi?)
✅ Macho na shungi (amefumba macho, shungi limepungua rangi?)
✅ Kuna mabadiliko yoyote ya karibuni? (chakula kipya, joto kali, chanjo, kusafirishwa?)

Kuku wawili wanaweza kuonekana wamezubaa lakini sababu zikawa tofauti kabisa:

• Mmoja ana stress ya joto
• Mwingine ana maambukizi
• Mwingine ana njaa, amedhulumiwa chakula, au amepungukiwa na maji

Kuwaita wote “wamezubaa” na kuwapa dawa ile ile ndiyo chanzo cha wafugaji wengi kukata tamaa.

Mfugaji mzuri si yule anayetoa dawa nyingi, bali ni yule anayechunguza kwa makini, anaeleza dalili kwa usahihi, na anawasiliana vizuri.

Kadiri maelezo yako yanavyokuwa bora, ndivyo suluhisho linavyopatikana haraka na kwa usahihi zaidi.

Kwa hiyo mara nyingine kuku wako anapokuwa hana uchangamfu, usihofu haraka.
Chunguza, andika dalili zote, kisha omba ushauri kwa uwazi.
Hatua hiyo pekee inaweza kuokoa banda lako.

K**A WEWE NI MFUGAJI MPYA, USIANZE NA LAYERS!Wafugaji wengi huingia kwenye ufugaji wa mayai wakitegemea faida za haraka,...
03/07/2026

K**A WEWE NI MFUGAJI MPYA, USIANZE NA LAYERS!

Wafugaji wengi huingia kwenye ufugaji wa mayai wakitegemea faida za haraka, lakini baadaye hukata tamaa kutokana na changamoto za usimamizi.

K**a ndio unaanza, anza na kuku wa kienyeji au chotara.

Kwa nini?

✅ Ni wastahimilivu zaidi dhidi ya mazingira.
✅ Hawahitaji usimamizi mgumu k**a layers.
✅ Ni rahisi kujifunza misingi ya ufugaji.
✅ Unaweza kupata faida kupitia nyama na mayai (kwa chotara).

Baada ya kupata uzoefu wa kutosha, ndipo unaweza kuingia kwenye ufugaji wa layers ukiwa na maarifa na ujasiri wa kusimamia mradi wako.

Farming also has its shortcomings like any other business,
03/07/2026

Farming also has its shortcomings like any other business,

25/06/2026

MAARIFA NI MSINGI WA BIASHARA YOYOTE

Ukitaka kufanya biashara yoyote, jambo la kwanza kabisa ni kuhakikisha unaifahamu kwa kina. Biashara haianzi na kusikia tu kwamba “hii inalipa”, bali inaanzia kwenye maarifa, taarifa sahihi na uelewa wa mazingira ya biashara husika.
Kukimbilia fursa bila kujifunza ni sawa na kuingia baharini bila kujua kuogelea.

Watu wengi wamepata hasara si kwa sababu biashara walizochagua ni mbaya, bali kwa sababu waliingia bila maandalizi. Mfano, mtu anasikia kuwa kilimo cha matikiti kinalipa, anaharakisha kununua mbegu na kulima bila kujifunza aina ya udongo unaofaa, msimu sahihi wa kupanda, gharama za uzalishaji, magonjwa ya mazao, soko na bei. Mwisho wa siku anavuna hasara badala ya faida.

Tatizo halikuwa matikiti, tatizo lilikuwa ukosefu wa maarifa.

Vivyo hivyo, ukitaka kufanya biashara ya duka, huwezi kufungua tu duka bila kujua kanuni za biashara hiyo. Ni lazima ujifunze aina ya bidhaa zinazotembea kwa eneo lako, bei za kununua na kuuza, namna ya kusimamia mtaji, hesabu za faida na hasara, pamoja na mbinu za kuhudumia wateja.

Bila elimu hiyo, duka linaweza kufungwa mapema licha ya kuwa na bidhaa nyingi.

Maarifa ya biashara yanakupa uwezo wa kufanya maamuzi sahihi, kupunguza hasara zisizo za lazima na kuongeza faida. Yanakusaidia kutambua hatari mapema, kupanga bajeti vizuri na kuona fursa ambazo wengine hawazioni.

Biashara bila maarifa ni k**a kuendesha gari usiku bila taa — ajali ni suala la muda tu.

Kwa hiyo, kabla ya kuanza biashara yoyote, jifunze. Tafuta taarifa, soma, hudhuria mafunzo, zungumza na walio kwenye biashara hiyo, elewa changamoto na uhalisia wake.

Maarifa hayazuii mafanikio, bali ndiyo yanayoyafungua. Kumbuka, si kila kinacholipa kwa mwingine kitakulipa bila wewe kujifunza kwanza.

Biashara bora hujengwa juu ya elimu, si juu ya porojo.

Ukiwa na mtaji wa TSh milioni 2, njia nzuri ya kuukuza kupitia kilimo cha mahindi ni kuanza na eneo unaloweza kulisimami...
21/06/2026

Ukiwa na mtaji wa TSh milioni 2, njia nzuri ya kuukuza kupitia kilimo cha mahindi ni kuanza na eneo unaloweza kulisimamia vizuri badala ya kulima eneo kubwa bila mtaji wa kutosha.

Mpango wa TSh milioni 2

Kukodi shamba (ekari 3): TSh 200,000
Mbegu bora za mahindi: TSh 150,000
Mbolea ya kupandia na kukuzia: TSh 600,000
Kulima, kupanda na palizi: TSh 400,000
Dawa na gharama nyingine: TSh 150,000
Jumla: karibu TSh 1,500,000

Lengo la uzalishaji

Kwa usimamizi mzuri, mahindi yanaweza kutoa wastani wa tani 2-4 kwenye hamna hamna kwa hekta katika maeneo mengi ya Tanzania, na zaidi kwenye maeneo yenye rutuba na matumizi sahihi ya pembejeo. �

Jinsi ya kukuza mtaji
Lima ekari 3 msimu wa kwanza.
Usiuze mara baada ya kuvuna k**a una sehemu ya kuhifadhi; bei mara nyingi huwa juu zaidi baada ya miezi kadhaa. �

Faida yote irudishe shambani msimu unaofuata.
Kutoka ekari 3 unaweza kuhamia ekari 5–8 ndani ya misimu 2–3 ukiendelea kuzungusha faid

Muhimu zaidi

Tumia mbegu bora.
Panda kwa wakati.
Fanya palizi mapema.
Tumia mbolea kwa kiwango sahihi.
Linda mazao dhidi ya viwavijeshi na magonjwa.

Mtu atauliza laki 5 Iko wap apo Kuna kitu inaitwa emergency na kuish tumia hyo ya juu.

Kipindi hiki cha Msimu wa mavuno, Kuna mchezo mchafu wa kisaikolojia unaofanyika sokoni hasa katika kipindi hiki  na wak...
19/06/2026

Kipindi hiki cha Msimu wa mavuno, Kuna mchezo mchafu wa kisaikolojia unaofanyika sokoni hasa katika kipindi hiki na wakulima wengi wanapoteza mamilioni bila kujua.

Madalali hawatumii nguvu, wanatumia saikolojia ya hofu (Fear-Based Pricing) kuwafanya wakulima wauze mazao yao kwa hasara mara tu wanapoyavuna.

k**a wewe ni Mkulima na yeyeto unae tamani kuingia kwenye hii shughuli ya kilimo soma Hadi mwisho post hii.

1. The Ghost Supply (Uhaba wa Kichawi)

Ukiwa bado upo shambani mkoani, unampigia simu dalali wa Ilala au Mabibo kuulizia bei.

Anakuambia
“Kiongozi, soko limefurika mno, malori yamepanga mstari tangu jana usiku, bei imeshuka hadi elfu”

Hofu inakuingia unapaniki unashusha bei ukiwa bado upo shambani ili usipoteze kila kitu.

Ukifika sokoni, unakuta soko lipo wazi na mzigo ni mchache.

2. The First Buyer Cartel (Mtego wa Mnunuzi wa Kwanza)

Gari lako la mazao likifika sokoni saa 11 alfajiri, anakuja mnunuzi wa kwanza anakupa ofa ya hovyo kabisa bei ya chini sana, mfano elfu 30 badala ya elfu 50. Ukimkatalia, anaondoka.

Anachofanya ni kwenda kuwaambia madalali wengine: “Yule jamaa wa gari la kijani msimpe zaidi ya elfu 25.”

Kila anayekuja baada ya hapo anakutajia bei ya chini zaidi, hadi unajuta kwa nini ulimkatalia yule wa kwanza.

Mwisho wa siku, unajikuta umeuza kwa hasara!

3. Artificial Quality Shaming (Kushusha Ubora wa Kisaikolojia)

Dalali akifika kwenye mzigo wako, haanzi kujadili bei anaanza kukagua mazao huku akikunja uso na kuguna.

“Mmh, mbona haya matunda yana unyevu sana? Mbona haya mahindi hayajakauka vizuri? huku sokoni haya hayaendi kiongozi.”

Lengo si kukataa mzigo wako wala si kwamba mzigo wako hamnazo
lengo ni kukuharibu kisaikolojia (emotional damage) ili ujione una bidhaa mbovu na ukubali bei yoyote atakayotaja, mradi tu uondoke!

4. The Delay Strategy (Mchezo wa Kutega Muda)

Hii huwakumba sana wanaolima mazao yanayoharibika haraka (horticulture) k**a nyanya na matango.

Dalali anakuacha ukae na gari lako sokoni tangu asubuhi hadi saa 10 jioni bila kukupa bei yoyote ya maana.

Anajua kabisa jua likizama huna sehemu ya kuhifadhi mzigo, na kesho yake mazao yataanza kuharibika ikifika saa 11 jioni, anakutajia nusu ya bei ya kawaida.

Kwa sababu huna namna nyingine, unamkabidhi mzigo kinyonge unarudi tunduru kusikilizia!

Mwisho wa yote kilimo ni biashara, kilimo ni fursa, msiache kuwekeza kwenye kilimo wakuu...................MWISHO

Kukohoa kwa Kuku: Dalili, Sababu, Tiba na Kinga 👇Kukohoa kwa kuku ni dalili ya kawaida ya muwasho au ugonjwa wa mfumo wa...
17/06/2026

Kukohoa kwa Kuku:
Dalili, Sababu, Tiba na Kinga 👇
Kukohoa kwa kuku ni dalili ya kawaida ya muwasho au ugonjwa wa mfumo wa upumuaji. Tatizo hili linaweza kuwapata kuku wa umri wowote, na likipuuzwa linaweza kuenea haraka ndani ya kundi, na kusababisha ukuaji hafifu, kupungua kwa uzalishaji wa mayai, na hata vifo katika hali mbaya.

1. Dalili za Kukohoa kwa Kuku
Zingatia dalili hizi 👇
👉 Kukohoa mara kwa mara au kutoa sauti k**a ya kukabwa koo.
👉 Kupiga chafya.
👉 Kutokwa na k**asi puani.
👉 Macho kutoa machozi au kuvimba.
👉 Kupumua kwa shida.
👉 Kupumua kwa mdomo wazi.
👉 Kupungua kwa ulaji wa chakula na maji.
👉 Ukuaji hafifu na kupungua uzito.
👉 Kupungua kwa uzalishaji wa mayai.
👉 Udhaifu na kutokuwa na uchangamfu.

2. Sababu za Kukohoa kwa Kuku
👉 Magonjwa ya mfumo wa upumuaji k**a Bronkaitisi ya Kuambukiza (Infectious Bronchitis), CRD, Ugonjwa wa Newcastle, na Koriza ya Kuambukiza (Infectious Coryza).
👉 Matandazo yenye vumbi na ukosefu wa uingizaji hewa wa kutosha.
👉 Mkusanyiko wa gesi ya amonia unaotokana na kinyesi chenye unyevunyevu.
👉 Mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa au baridi kali.
👉 Chakula kilichoshika ukungu au matandazo yaliyochafuliwa.
👉 Msongamano mkubwa wa kuku ndani ya banda.
👉 Kukaribiana na moshi, kemikali au viuatilifu vyenye harufu kali.

3. Tiba za Asili kwa Kuku Wanaokohoa
👉 Ongeza kitunguu saumu kilichosagwa kwenye maji ya kunywa ili kusaidia kuimarisha kinga ya mwili.
👉 Changanya juisi ya tangawizi kwenye maji ili kusaidia kusafisha njia za hewa.
👉 Wape majani mabichi ya mwarobaini au moringa k**a virutubisho vya ziada.
👉 Hakikisha wanapata maji safi na ya kutosha kila siku.
👉 Boresha uingizaji hewa ndani ya banda na ondoa matandazo yenye unyevunyevu mara moja.
👉 Watenge kuku walioathirika ili kupunguza kuenea kwa maambukizi.
👉 Punguza vumbi na hakikisha banda linakuwa safi muda wote.

4. Namna ya Kuzuia Kukohoa kwa Kuku
👉 Hakikisha banda lina uingizaji hewa mzuri.
👉 Epuka msongamano mkubwa wa kuku.
👉 Badilisha matandazo yenye unyevunyevu mara kwa mara.
👉 Fuata ratiba sahihi ya chanjo.
👉 Wape lishe bora na maji safi kila wakati.
👉 Watenge kuku wapya kabla ya kuwaingiza kwenye kundi.
👉 Safisha na kuua vijidudu kwenye vifaa vya kufugia mara kwa mara.
👉 Punguza msongo unaosababishwa na joto kali au baridi kali.
👍 Utambuzi wa mapema na usimamizi mzuri wa kundi ni njia bora za kuzuia kukohoa kwa kuku na kuwafanya wabaki na afya njema, wazalishe vizuri na wakue ipasavyo.

Athari za Minyoo kwa Kuku::::Minyoo ni mojawapo ya matatizo yanayoathiri afya na uzalishaji wa kuku. Minyoo huishi ndani...
16/06/2026

Athari za Minyoo kwa Kuku::::

Minyoo ni mojawapo ya matatizo yanayoathiri afya na uzalishaji wa kuku. Minyoo huishi ndani ya utumbo wa kuku na kutumia virutubisho vinavyopaswa kusaidia ukuaji wa ndege hao. Endapo tatizo hili halitatambuliwa na kutibiwa mapema, linaweza kusababisha hasara kubwa kwa mfugaji.

1. Kupungua kwa ukuaji wa kuku: Kuku wenye minyoo hukua taratibu kwa sababu virutubisho vingi hutumiwa na minyoo badala ya mwili wa kuku.

2. Kupungua kwa uzito: Kuku wanaweza kula vizuri lakini wakaendelea kukonda kutokana na minyoo kunyonya chakula walichokula.

3. Kushuka kwa uzalishaji wa mayai: Kwa kuku wa mayai, minyoo inaweza kusababisha kupungua kwa idadi na ubora wa mayai yanayozalishwa.

4. Kukosa hamu ya kula: Baadhi ya kuku walioathirika huonyesha dalili za kula chakula kidogo au kutokula kabisa.

5. Kuharisha: Minyoo inaweza kusababisha kuharisha, wakati mwingine kinyesi huonekana kuwa na ute au hata minyoo wenyewe.

6. Kulegea na udhaifu: Kuku wenye minyoo mara nyingi huonekana wachovu, wasiochangamka na hupunguza shughuli zao za kawaida.

7. Upungufu wa damu: Baadhi ya aina za minyoo hunyonya damu, hali inayoweza kusababisha kuku kuwa na upungufu wa damu na masega kuwa meupe.

8. Kushuka kwa kinga ya mwili: Minyoo hudhoofisha mfumo wa kinga, hivyo kuku kuwa rahisi kushambuliwa na magonjwa mengine.

9. Vifo kwa maambukizi makubwa: Endapo idadi ya minyoo ni kubwa sana, inaweza kuziba utumbo na kusababisha vifo vya kuku.

10. Hasara za kiuchumi kwa mfugaji: Matumizi ya dawa, kupungua kwa uzalishaji na vifo vya kuku husababisha hasara katika biashara ya ufugaji.

Namna ya kuzuia minyoo kwa kuku:
Wape kuku dawa za minyoo kulingana na ushauri wa mtaalamu wa mifugo.
Dumisha usafi wa banda na badilisha matandazo mara kwa mara.
Epuka msongamano mkubwa wa kuku.
Osha vyombo vya chakula na maji kila siku.
Tenga kuku wagonjwa na uwafuatilie kwa karibu.
Kinga na uchunguzi wa mapema ni njia bora ya kulinda afya ya kuku na kuhakikisha uzalishaji mzuri katika shamba lako.

Address

P. O. BOX 163 NJOMBE
Njombe

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Agriworth Tanzania Company ltd posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category