MAMBO MSETO

MAMBO MSETO This page is for mixed and informative information.

Wanafunzi wa Kidato Cha nne wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Green Star wakiimba wimbo wa kuwapongeza wahitimu wa D...
30/08/2025

Wanafunzi wa Kidato Cha nne wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Green Star wakiimba wimbo wa kuwapongeza wahitimu wa Darasa la Saba wa Shule ya Msingi ya Green Star katika Mahafali ya Tisa ya darasa la Saba na mahafali ya Kumi na Mbili ya darasa la awali ya Shule za Green Star wilayani Kahama.

Wahitimu wa darasa la Saba wa Shule ya Msingi ya Green Star wakiimba wimbo maalumu wa kuaaga katika  Mahafali ya Tisa ya...
30/08/2025

Wahitimu wa darasa la Saba wa Shule ya Msingi ya Green Star wakiimba wimbo maalumu wa kuaaga katika Mahafali ya Tisa ya darasa la Saba na mahafali ya Kumi na Mbili ya darasa la awali ya Shule za Green Star wilayani Kahama.

NI MAHAFALI YA TISA YA DARASA LA SABA NA MAHAFALI YA KUMI NA MBILI YA DARASA LA AWALI YA SHILE ZA GREEN STAR WILAYANI KA...
30/08/2025

NI MAHAFALI YA TISA YA DARASA LA SABA NA MAHAFALI YA KUMI NA MBILI YA DARASA LA AWALI YA SHILE ZA GREEN STAR WILAYANI KAHAMA, VIJANA WAKIONESHA JINSI WANAVYOVITENDEA HAKI VIPAJI VYAO KWA KUONESHA BURUDANI MBALIMBALI

21/01/2023

KAHAMA YAOMBWA KUTENGA ENEO LA KILIMO CHA VANILLA.

MKURUGENZI wa Kampuni ya Vanilla International, Saimon Mkondya, ameipongeza Serikali kuondoa Kodi kwa zao la Vanilla huku akiomba wilaya ya Kahama kutenga eneo la kilimo Cha zao hilo.

19/01/2023

KAHAMA KULIMA ZAO LA VANILLA

Wakazi wa wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, wameaswa kukuza uchumi wa kaya zao kwa kujikita kulima zao la biashara la Vanilla ambalo lina soko kubwa Duniani.

Ushauri huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ihusikanayo na zao hilo nchini, Saimoni Mkondya, huku akiwasisitiza kwa ustawi wa vyakula walime mazao mengi ya chakula, huku wakihamasika kulima zao la Vanilla.

KWA TANZANIA YANGA NI KUBWA KULIKO SIMBA LAKINI MKUBWA ANADEKEZWA KULIKO MDOGO. KWA NINI?YANGA imeanzishwa kabla ya Simb...
13/09/2022

KWA TANZANIA YANGA NI KUBWA KULIKO SIMBA LAKINI MKUBWA ANADEKEZWA KULIKO MDOGO. KWA NINI?

YANGA imeanzishwa kabla ya Simba. Wameshinda ubingwa wa nchi hii mara nyingi kuliko Simba. Kwenye ubingwa wa nchi wameifunga Simba mechi nyingi na magoli mengi zaidi ya Simba ;ANAANDIKA IBRAHIM MKAMBA.

Kwa takwimu hizo, kwa hapa Tanzania, Yanga ni wakubwa wa Simba,lakini kinachoshangaza, mara nyingi Yanga hudekezwa k**a vile wao ndiyo wadogo! Jambo ambalo hata wenyewe hawalilalamikii,ajabu hupata walalamikaji kibao kwenye media!

Ushahidi wa hili tafakari maneno yaliyosemwa sana kwamba kocha Mkuu wa muda wa Simba, Juma Mgunda hakuwa na cheti cha kumruhusu kusimamia timu kwenye mashindano ya CAF na baadaye mmoja akasema kocha Nasredeen Nabi wa Yanga naye hakuwa na cheti hicho. Baadaye ilibainika kuwa maneno kuwahusu wataalam hao hayakuwa ya ukweli.

Jambo la kushangaza ni kwamba aliyemsema hivyo Nabi amejiwa juu mno huku akishinikizwa aombe radhi lakini waliomsema Mgunda hawakutani na shinikizo lolote! Hii naona ni sawa na udekezaji.

Yanga waachwe wawe wanapotezea baadhi ya vitu ili akili zao zifikirie makubwa yanayolingana na ukubwa wao. Kuwalalamikialalamikia kwa mambo ambayo wenyewe hawayalalamikii kunawalazimisha wapeleke sehemu ya akili zao huko bila umuhimu wowote.

Imebainika wote Mgunda na Nabi wanavyo vyeti vinavyowawezesha kusimamia mechi za CAF, si basi. Cha msingi ni kusisitiziana kutangaza mambo baada ya kuwa na uhakika nayo.

Msiwe mnakuza sana mambo ya kawaida ya kuikera Yanga kutafsiri kuna watu wana chuki nao. Hii itawaathiri hao Yanga kisaikolojia na kinyume chake inawafanya Simba wawe imara kukabili hali ya kusemwasemwa vibaya bila utetezi wa mtu yeyote.

La Nabi linapaswa limalizike k**a lilivyomalizika la Mgunda kuhusu vyeti vyao vya CAF. Kubwa ni kukumbushana kuwa taatifa za uongo za kuchafua hadhi za watu zinaweza siku moja zikasababisha mtu afilisiwe kwa kupitia kesi Mahak**ani. Tujihadhari kabla ya hatari.

YANGA WAMEYASHINDA MAZOEA TANZANIA BARA K**A ARSENAL WATAKAVYOYASHINDA ENGLANDYANGA walikosa ubingwa Tanzania Bara msimu...
24/08/2022

YANGA WAMEYASHINDA MAZOEA TANZANIA BARA K**A ARSENAL WATAKAVYOYASHINDA ENGLAND

YANGA walikosa ubingwa Tanzania Bara msimu wa 2020/2021 baada ya kuongoza ligi kwa kipindi fulani. Ni msimu huo ndipo walipopoteza mechi ya mwisho ya ligi kuu ya Tanzania Bara mpaka sasa kwa kufungwa 1-0 na Azam FC. Kisha wak**aliza mechi saba zilizobaki msimu huo bila kupoteza mechi. Simba wakabeba ubingwa wa nne mfululizo msimu huo.ANAANDIKA IBRAHIM MKAMBA.

Hali hiyo ya Yanga kuongoza ligi kipindi fulani kisha kukosa ubingwa ilikuwepo pia huko nyuma Simba wakiibuka mabingwa katika misimu hiyo ya ubingwa wao wa mfululizo wa miaka minne. Baadhi ya watu wakajenga mazoea kwamba Yanga ni wa kuongoza ligi na ubingwa ni wa wengine k**a Simba.

Ukaja msimu wa 2021/2022, baadhi wakaendelea kuishi na mazoea yale yale kwamba Yanga wataongoza ligi lakini ubingwa utakuwa wa Simba. Watu kadhaa wakaimba wimbo huo kwa muda mrefu huku Yanga wakiongeza idadi ya mechi za kushinda, idadi ya mechi za kutopoteza, idadi ya magoli ya kufunga na kuruhusu mabao machache ya kufungwa.

Wakabeba ubingwa na rekodi ya kutopoteza mechi zote 30 za ligi kuu za msimu. Ukiongeza saba za msimu uliopita, zikafika mechi 37 bila kupoteza mechi na sasa zimefika 39! Wasipopoteza kwa Azam mechi inayofuata, watafikisha 40. Kumbuka Azam hiyo ndiyo timu ya mwisho kuishinda Yanga kwenye ligi kuu Tanzania Bara.

Kwa hiyo, kwa hapa Tanzania Bara, msimu uliopita, Yanga walishinda mengi yaliyoelezwa hapo juu ukiwemo ushindi mkubwa dhidi ya mazoea ya kwamba wataongoza ligi, ubingwa utakuwa wa wengine. Waliyashinda mazoea hayo kwa kuongoza ligi na kutwaa ubingwa.

Tunawasikia wanaozungumzia soka ya England wakiimba wimbo huo huo wa mazoea eti Arsenal watakuwa juu k**a ilivyotokea misimu kadhaa nyuma lakini si tu watakosa ubingwa bali hata nne bora hawatapata!

Hapana, tuache kuishi kwa mazoea. Arsenal hii huko England itayashinda mazoea dhidi yao k**a Yanga walivyoyashinda hapa Tanzania Bara. Take it from me.

WAPINZANI WA YANGA LIGI YA MABINGWA WAPATA MCHECHETOWapinzani wa Yanga kwenye hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika, Za...
23/08/2022

WAPINZANI WA YANGA LIGI YA MABINGWA WAPATA MCHECHETO

Wapinzani wa Yanga kwenye hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika, Zalan FC ya Sudan ya Kusini,Ni K**a wameingiwa na mchecheto juu ya michuano hiyo baada ya kuamua kuvunja benchi la ufundi na kuunda jipya.

Hatua hiyo ilifikiwa juzi na timu hiyo zikiwa zimebaki siku chache kukutana na mabingwa wa Kihistoria nchini Tanzania, Yanga kwa kumtambulisha kocha mpya, Baping Alliab.

Alliab ambaye amewahi kuwa Kocha wa Al Hilal Wau Sudan Kusini na kubeba Kombe la Ligi ataiongoza Zalan kwenye mechi za Afrika ambapo mchezo wa kwanza utapigwa kati ya Septemba 9 hadi 11 huku marudiano ikichezwa Septemba 16 mpaka 18.

Mshindi wa jumla baina ya klabu hizo atacheza na mshindi kati ya St.Georges ya Ethiopia na Al Hilal ya Sudan.

“Uongozi wa Zalan FC unathibitisha kumteua Baping Aliap k**a kocha mkuu wa Zalan FC kwa kipindi cha mwaka mmoja (1) ikitegemea kumuongeza mkataba kutokana na kiwango timu itakachoonyesha,” ilisema taarifa ya klabu hiyo.

Kocha huyo msimu uliopita alikuwa anakinoa kikosi cha Al Hilal Wau ambapo waliibuka Mabingwa wa Sudan Kusini

NI LAZIMA MWANAUME KUFANYA MAPENZI NA MAMA MWENYE NYUMBA PINDI ATEMBELEAPO KABILA HILI.BARANI Afrika Kuna makabila ambay...
19/08/2022

NI LAZIMA MWANAUME KUFANYA MAPENZI NA MAMA MWENYE NYUMBA PINDI ATEMBELEAPO KABILA HILI.

BARANI Afrika Kuna makabila ambayo licha ya kuwepo utandawazi uliotamalaki Duniani, yameendela kulinda Mila na desturi zao na kuepuka kuiga ustaarabu utokao nchi za ughaibuni kwa hofu ya kulaaniwa na mababu zao.

Miongoni mwa jamii zinazoendeleza Mila zao toka Karne na Karne, pasipo kuathiriwa na utandawazi uliopo ni Kabila la Himba, linalopatikanakatika eneo la Kunene nchini Namibia.

Licha ya kabila hili kuendelea kuvunja rekodi ya uchafu,kunakosababishwa na uhaba wa maji, jamii ya kabila Hilo huwakarimu wageni wa kiume wanaofika kwenye boma zao kwa kushiriki nao tendo la ndoa.

Watu hao wanaoishi katika milima ya Himalaya, hupamba watoto wao wachanga kwa shanga za kiunoni. Maisha yao wanaishi kwa kujitenga na wanaogopa kuwasiliana na watu wa nje.

Jamii hii ya watu wa Himba, wengi wao hujishughulisha na KILIMO na ufungaji hutekeleza majukumu Yao ya kuwaingizia kipato kwa bidii ili kuhakikisha kwamba imani na utamaduni wao hauchafuzwi na watu wa nje.

Shughuli za Kilimo na ufugaji kwa asilimia kubwa hutekelezwa na wanaume huku Wanawake wao wakijishughulisha na kukusanya kuni, kupika na kuandaa chakula na kutafuta maji yasiyo na chumvi.

Ndoa za wake wengi ni kawaida na wasichana huozwa wakiwa na umri mdogo, watu hawa wa Himba wanaishi katika mojawapo ya mazingira ya ukame, hali mbaya ya hewa ya jangwani na ukosefu wa maji ya kunywa ni sababu za kabila hili kupata shida ya kuoga.

Kinachofurahisha zaidi wanawake wa kabila hili wanaoga siku ya harusi tu, mbaya zaidi mgeni anapoingia kwenye kabila anatakiwa kulala na mke wa mwenyeji kuonesha ukarimu.

Address

Majengo, Kahama
Shinyanga

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when MAMBO MSETO posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to MAMBO MSETO:

Shortcuts

Share

Category