20/07/2024
Ulikuwa ni Wasaa Mzuri kushiriki katika Zoezi la Kujenga Chama chetu ambapo tulismamia zoezi zima la Usajili wa Wanachama kwa Njia ya Electroniki ili kupata Kadi za Kimtandao Wilaya ya Mkuranga.
Kwa dhati kabisa ningependa kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu Mwingi wa Rehma kwa Rehma zake na kutufanya tuanze na kumaliza zoezi letu kwa kufanikiwa kwa Asilimia zote.
Lakini pia shukrani zimuendee Mwenyekiti wetu na Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha kwamba Ccm inahama kutoka kwenye mfumo wa Kadi za Ganda kuelekea kwenye Kadi za Kieletroniki hii ni hatua kubwa sana.
Katika zoezi letu tulikumbana na Changamoto sana lakini kwa kuwa tuna Viongozi Imara Mkuranga chini ya Mwenyekiti wetu Alhaji Magaila, imepelekea kufanya zoezi letu kwenda vizuri richa ya Changamoto ndogondogo. Lakini pia Mheshimiwa Mkuu wetu wa Wilaya Dada yetu Khadija Nassir Ally amekuwa na sisi Bega kwa Bega kuhakikisha Zoezi letu linakwenda Vizuri.
Kwa dhati Kabisa shukrani zimuendee Mbunge wetu wa Jimbo la Mkuranga ambae pia ni Waziri wa Mifugo ma Uvuvi Mhe Alhaji Abdallah H. Ulega kwa kujitoa kwake kutusaidia vifaa mbalimbali ili vitusaidie katika Kutekeleza Zoezi letu vizuri bila ya Kukwama, hivyo pamoja na yote shukrani pia zimuendee Mbaraza na Mjumne wa Kamati ya Utekelezaji wa Umoja wa Wanawake Tanzania anaetokea Mkoa wa Pwani Mhe Mariam Ibrahim Ulega kwa Mchango wake Katika Zoezi hili mpaka kufikia Tamati.
Zoezi hili limefanywa na Sisi Vijana Chini ya Mwenywkiti wetu wa Vijana wa Wilaya, Kaka yetu Mohamed Kizundu ,hivyo Hamasa na Ari tuliyopata na kutupelekea kufanya kazi vizuri ilitoka kwa Kaka yetu Mwenyekiti wetu Bingwa kabisa.
Lakini haya yote tusingeyatekeleza kwa ufanisi bila ya kuwa na Timu Imara, hivyo tulikuwa na Timu ya Vijana Makini na Imara.