Tanzania Food System Resilience Program - Zanzibar

Tanzania Food System Resilience Program - Zanzibar Huu ni mradi ambao umefadhiliwa na World Bank

20/01/2025

Afisa Kiungo wa Mradi wa Uhimilivu wa Mifumo ya Chakula Tanzania Mohamed Faida Haji amesema ni vyema kwa wakulima kufuatilia bei za mboga mboga kabla ya kuanza shughuli zao za kilimo ili kuepuka kupungua kwa bei za mazao .
Ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kutembelea soko la mwanakwerekwe ikiwa ni muendelezo wa kuwajengea uwezo kwa vitendo mabwana na Mabibi shamba ili kuhamasisha wakulima kulima Kilimo chenye tija na kuinua uchumi.
Amesema kupitia dhana ya mbinu shirikishi ya kuwawezesha wakulima katika suala la Uzalishaji itawasaidia kujua gharama za Uzalishaji wa Mazao yao kabla ya kuuza sokoni.
Aidha amesema kuna Changamoto kubwa kwa Wakulima wengi huzalisha mazao kwa Mkumbo jambo ambalo huleta hasara pindi wanapoyafikisha masokoni hivyo amewashauri wakulima wanapoyapeleka biashara masokoni kuuliza bei za mazao na kuelewa bidhaa zipi zinahitajika sokoni kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na mazao mengine kutokana na kuwepo kwa tatizo la kuzalisha mazao mengi kwa kipindi kimoja
Kwa upande wake Mtaalam wa Kilimo Cha Mazao ya Bustani na Mkufunzi wa mafunzo hayo Masumbuko M***a Weswa ameeleza kuwa ni muhimu kufuata njia za kitaalamu kwa wakulima ili kuimarisha kilimo na kuacha Kilimo Cha mazowea na kulima Kilimo Cha biashara .
Nae Afisa Kilimo Wilaya ya Magharibi "B" Husna Khamis Suleiman amesema kutokana na mafunzo waliyopewa ameahidi kuyafanyia kazi mafunzo waliyopewa sambamba na kuwaelimisha Wakulima ili waweze kulima Kilimo Cha kisasa cha kuongeza tija.
Nae Mfanyabiashara wa zao la pilipili boga Mohamed Said Abdalla kwa niaba ya wafanyabiashara wenziwe wamesema kwa sasa Kilimo cha mboga mboga kinazalishwa kwa wingi ukilinganisha na Zamani hususani kilimo Cha tungule hivyo wamesema wakulima wafuatilie miongo ambayo mazao hayo Huwa hafifu masokoni na kutumia njia imara ili kuimarisha bidhaa hizo.

09/01/2025
Mratibu wa Mradi wa Uhimilivu wa Mifumo ya Chakula Tanzania Zanzibar Sihaba Haji Vuai (kidume), akifungua Mafunzo ya kuw...
09/01/2025

Mratibu wa Mradi wa Uhimilivu wa Mifumo ya Chakula Tanzania Zanzibar Sihaba Haji Vuai (kidume), akifungua Mafunzo ya kuwajengea Uwezo juu ya Upatikanaji wa Masoko kwa mabibi Shamba na mabwana Shamba pamoja na Maafisa Ushirika kutoka Wilaya mbali mbali za Unguja, ambapo hafla hiyo imefanyika huko katika Ukumbi wa Wizara ya Kilimo Maruhubi.

Address

Maruhubi
Zanzibar City

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanzania Food System Resilience Program - Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category