20/01/2023
1.NITAUTAFUTA USO WA BWANA.
Kitu kinacho tafutwa, maranyingi ni kile kilichopotea. K**a ni hivyo basi, je sisi tumepoteza uso wa Bwana?
"k**a ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja. Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja."
Warumi 3:10-12
Ndiyo, wanadamu wote tumepoteza uso wa Bwana, na nihitaji letu sote.
Kwani sura ya Mungu katika maisha yetu ni nini basi?
"Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni."Mwanzo 4:16
Kaini baada ya dhambi aliyo itenda "alitoka" yani aliondoka au hakufaa kuwapo tena "usoni pa Bwana". Uso wa Bwana ni ushirika tupatao wanadamu kwa Bwana. Ni haki, uhakika, na amani juu ya uzima wa milele.
"Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya."
1 Petro 3:12
Kwanini uso/urafiki wa kimbingu huu uwe juu ya watendao mabaya?
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."
Yohana 3:16
Ushirika huu uko juu ya sisi tutendao mabaya ili tusipotee, bali tuwe na nafasi ya kujiunga nao, uso wa Bwana uonekane katika maisha yetu mwisho wa nyakati tupate uzima wa milele.
JE, NAWEZA UTAFUTA TENA USO WA BWANA KATIKA MAISHA YANGU?
Jibu ni ndiyo waweza nami pia naweza.
Tujifunze kwa watu waliopoteza uso wa Bwana na wakautafuta tena.
1. Israeli wakati wa sauli aliye waua wagibeoni, ambao Israel waliwaapia kuto waua. Bwana aliutoa ushirika na taifa hili, muda wa miaka mitatu wakati wa Daudi hakukuwa na mvua katika Israel, mpaka mfalme mcha Mungu Daudi alipoamua "kuutafuta uso wa Bwana" ndipo Bwana alipo mwambia kosa lao ninini, na nini wakifanye k**a taifa, walipofanya hayo ushirika wao na Mungu ulirejea tena. 2 samweli 21:1-
2. Yona nabii wa Mungu alipotumwa aende ninawi, akakimbia uso wa Bwana kwenda Tarshishi, Bwana mwenyewe alimrudisha katika ushirika kwa namna ya ajabu. Yona 1:3-.
3. Petro mtume wa Yesu alipopoteza uso wa Bwana kwa kumkana mara tatu, alipoamua kutubu na kuungama dhambi yake, Bwana alimkubali na kumsamehe kabisa.